*Ni majibu ya Manara baada ya kuibuka tetesi za kuondolewa usemaji wa Simba

Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu

MSEMAJI wa Klabu ya Simba Haji Manara amewaambia mashabiki na wapenzi wa soka nchini Tanzania kwamba kwa sasa yeye ndio Msemaji wa klabu hiyo na wala hakuna mwingine huku akieweka wazi hata hivyo hatakaa katika nafasi hiyo milele.

Manara amesema hayo leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari wakati anazungumzia mechi yao ya marudiano dhidi ya timu ya UD Songo itakayochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili ya wiki hii.

Baada ya kuzungumzia mechi hiyo na maandalizi ambayo wameyafanya,ukafika wakati wa maswali ambapo Mwandishi wa Michuzi Blogu alitaka kufahamu kuhusu nafasi ya Manara hasa baada ya kuwepo kwa tetesi zinazodai nafasi yake imechukuliwa na mtu mwingine.

Hivyo wakati anajibu swali hilo Manara alianza kwa kujibu hivi "Why Manara. Kwanini ,Why Manara na kama nafasi Simba mbona zimetangazwa nyingi tu iweje kwa Manara.

"Ngoja niwaambie kwa sasa Msemaji wa Klabu ya Simba ni Haji Sande Ramadhan Manara.Mimi ndio msemaji wa Simba na wala hakuna mwingine,"amesema Manara.

Wakati anajibu swali hilo Manara alionesha kuzungumza kwa utulivu na umakini mkubwa huku akifafanua licha ya kuwa yeye ndio Msemaji wa Simba lakini hatakaa milele katika nafasi hiyo na hilo amekuwa akilieleza mara kwa mara.

"Hata hivyo sijui kwanini watu wanazungumzia sana kuhusu nafasi yangu. Why ? Niwaambie ndugu zangu waandishi wa habari hakuna mtu mkubwa ndani ya Simba zaidi ya Simba yenyewe.Simba ni kubwa kuliko mtu yoyote.

"Najua kuna siku atakuja mwingine na akitoa wana Simba naomba tumpe ushirikiano mkubwa kama ambavyo mmekuwa mkinipa mimi,"amesema Manara.

Ametumia nafasi hiyo kueleza wazi anachofurahi zaidi hana tatizo lolote na uongozi wa Simba na wala hajaaambiwa chochote na ndio maana anaendelea kuchapa kazi na wanaoweka maneno mitandaoni wafahamu bado yupo yupo sana katika nafasi hiyo ya usemaji.

Kwa siku kadhaa sasa kwenye mitandao ya kijamii kumekuwepo na tetesi nyingi zinazodai kuwa Manara ameondolewa kuwa Msemaji wa Simba na badala yake atapewa kitengo cha hamasa. Ambapo katika hilo Manara amesema kuna mambo ya ajabu, kwani tetesi za uongo zinawekwa mitandaoni halafu viongozi wa Simba ndio wanatakiwa kujibu.

"Haya zaidi ya swali hili kuna tetesi gani nyingine za huko mitandaoni nizijibu? Aliuliza Manara kwa kujiamini huku akisisitiza yeye ndio Msemaji wa Simba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...