Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe kwa niaba ya Wizara leo, ametiliana saini ya makubalianao ya kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa masuala ya Kilimo Misitu (International Centre for Research in Agro-Forest - ICRAF). Taasisi ya ICRAF imekwa ikifanya tafiti zinazolenga kuboresha uhifadhi wa mazingira na uzalishaji wa nishati jadidifu ambayo ni muhimu katika shughuli za kilimo. 

Akizunzungumza baada ya kusaini hati za makubaliano Katibu Mkuu, Mhandisi Mtigumwe amesema kimsingi Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo imesahini makubaliano kwa ajili ya lengo la kushirikiana na ICRAF kwenye maeneo ya ugunduzi wa misitu inayopatikana kwenye ikolojia maalum, usimamizi wa misitu kwa lengo la kuongeza tija kwenye eneo hilo. 

Mhandisi Mtigumwe ameongeza kuwa Wizara itashirikiana na ICRAF katika eneo la ufuatiliaji wa madhara kwenye afya ya udongo, mabadiliko ya tabianchi kwenya ardhi ya kilimo ili kufanya tafiti zitakazokuja na majibu ya changamoto katika maeneo hayo. 

Mhandisi Mtigumwe ameongeza kuwa eneo moja la ushirikiano ni kujengeana uwezo wa kitaasisi pamoja na kubadilishana Wataalam, uzoefu katika tafiti mbalimbali pamoja na kubadilishana vinasaba vya mimea na mazao ya kilimo na misitu. 

Akiongea kwa niaba ya Taasisi ya ICRAF, Bi. Catherine Muthuri ambaye ni Msimamizi wa Shughuli la Taasisi hiyo iliyopo Jijini Nairobi amesema Tanzania na Kenya ni majirani wa muda mrefu na kwamba changamoto zinazowakuta Wakulima wa Kenya, zinawakuta pia na Wakulima wa Tanzania na kusisitiza kuwa lengo la nchi hizi mbili ni kuhakikisha mambo mazuri kama ya kushirikiana katika tafiti; yanafanyika kivitengo kwa lengo la kuboresha Sekta ya Kilimo.

Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe kushoto kwa niaba ya Wizara akimkabidhi hati ya makubaliano ya kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya ICRAF mara baada ya kusaini ya makubalianao ya kushirikiana kulia ni Msimamizi Mkuu wa Taasisi hiyo Bi. Catherine Muthuri, katika Ofisi za Wizara ya Kilimo katika eneo la Mtumba, Jijiji Dodoma leo tarehe 16/08/2019.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...