Na Karama Kenyunko Michuzi Tv.,

ASKARI Polisi watano na Mwanajeshi mmoja wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi yenye mashtaka matatu likiwamo la wizi wa mafuta ya ndege na Utakatishaji wa zaidi ya Sh. Milioni nne.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Koplo Shwahiba(38), MT. 74164 SGT Ally Chibwana (47), wa jeshi la wananchi Tanzania, PC Elidaima Paranjo (38), PC Simon (28), PC Dickson na PC Hamza.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa na wakili wa serikali , Faraji Nguka akisaidiana na Saada Mohammed mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Mwaikambo imedai washtakiwa wote hao wakiwa ni watumishi wa umma walikiuka maadili ya kazi zao na kupanga genge la uhalifu na kuiba lita 2180 za mafuta ya ndege( Jet A-1/Ik yenye thamani ya sh. 4,647,760.

Katika shtaka la pili imedaiwa, Julai 30,2019 huko katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere uliopo katika Wilaya ya Ilala jijini Darvea Salaam, watuhumiwa hao(askari), waliiba lita 2180 za mafuta ya ndege( Jet A-1/Ik yenye thamani ya sh. 4,647,760 malibya shirika la ndege Tanzania ATCL

Katika shtaka la pili imedaiwa, siku na mahali hapo washtakiwa hao wote walifanya uwizi wa mafuta hayo na kutakatisha kiasi hicho cha sh. Milioni 4.6 ambapo walikuwa wakijua kiwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la wizi kinyume na Sheria.

Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo husikilizwa mahakama kuu au pale DPP atakapotoa kibali cha mahakama hiyo kusikiliza.

Washtakiwa hao ambao wanatetewa na wakili Hasaan Kiangio wmerudishwa rumande hadi Septemba 24 mwaka huu kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...