Benki ya NBC imeratibu kongamano maalum la kibiashara kwa ajili ya wateja wake wadogo na wakati jijini Dodoma ambalo pamoja na mambo mengine lililenga kuwaongezea wateja hao hao uelewa kuhusiana na mabadiliko ya kihuduma na fursa za kiuwezeshaji kutoka benki hiyo.

Akizungumza wakati wa kongamano hilo lililofanyika hivi karibuni jijini humo, Meneja Ukuzaji wa Biashara Kitengo cha biashara ndogondogo na za kati wa Benki hiyo, Bw Jonathan Bitababaje alisema kufuatia uboreshwaji mkubwa wa huduma za benki hiyo ambazo zinaendana na kasi ya kiteknolojia na fursa za kiuchumi kumekuwa na hitaji kubwa kwa wateja hao kujengewa uelewa ili waweze kwenda sambamba na mabadiliko hayo.

“NBC kwasasa tumefanya mabadiliko makubwa ya kihuduma yanayoendana na kasi ya kiteknolojia na ukuaji wa uchumi na tumeona kuwa mabadiliko haya yatakuwa na tija zaidi kwa wateja wetu hasa wadogo na wakati ikiwa tu tutawajengea uelewa wa kutosha ili waweze kwenda sambamba mabadiliko haya badala ya kuwa changamoto,’’ alibainisha.

Alisema mbali na kuwajengea uelewa kuhusu huduma za benki hiyo,kupitia kongamano hilo washiriki waliweza kutoa maoni yao ikiwa ni mrejesho wa huduma wanazopata kutoka benki hiyo, hatua aliyosema itasaidia taasisi hiyo kuboresha zaidi huduma hizo sambamba na kubuni huduma mpya zinazoendana na mahitaji ya wateja hao.

Aidha katika kongamano hilo la siku moja, mbali na masuala ya kibenki washiriki walipata fursa ya kusikiliza na kuchangia mada kutoka kwa wawakilishi wa taasisi nyingine ikiwemo Chemba ya biashara, viwanda na kilimo (TCCIA)na Baraza la Uwezeshaji (NEEC) ambao walielezea fursa mbalimbali za kibiashara ndani na nje ya nchi ikiwemo nafasi ya taasisi hizo katika kuwaunganisha wafanyabiashara na wenzao kutoka nje ya nchi.

“ Kwa kushirikiana na benki ya NBC tumekuwa tukishirikiana mambo mengi yanayolenga kuwasaidia wafanyabiashara wetu na hivi karibuni tunatarajia kuwasafirisha wafanyabiashara kwenda nchini China kwa ajili ya safari ya kibiashara ya siku kumi ambapo wahusika watalipa gharama ya kiasi cha Dola za Kimarekani 2500 tu ambayo itagharamia mahitaji yao yote ya msingi ikiwemo nauli ya kwenda na kurudi, gharama za chakula na huduma nyingine ikiwemo ya wakalimani,’’ alisema Bw Patrick Magai, Meneja Maendeleo Viwanda kutoka TCCIA.

Wakizungumza wakati wa kongamano hilo lililofutiwa na Uzinduzi wa Klabu wa Wafanyabiashara ya Benki hiyo mkoani humo, baadhi ya washiriki walisema pamoja na huduma za kifedha ipo haja ya taasisi za kifedha hapa nchini kuongeza ushirikiano zaidi na wafanyabiashara hao pindi wanapotafuta zabuni kubwa zenye kuhitaji dhamana kutoka taasisi hizo.

“Pia ipo haja kwa taasisi za fedha nchini kutambua baadhi ya changamoto zinazotukabili wateja wao kwenye biashara zetu kwa kubuni huduma zinazotambua changamoto zetu ikiwemo kuangalia namna ya kushirikiana nasi pindi tunapokabiliwa na changamoto ya ucheleweshwaji wa malipo yetu kutoka kwa wateja wetu,’’ alisema mmoja wa wafanyabiashara hao ambae ni Mkandarasi, Dr Steven Masangia.


Meneja Ukuzaji wa Biashara Kitengo cha biashara ndogondogo na za kati wa Benki hiyo, Bw Jonathan Bitababaje akiwasilisha mada kuhusiana na huduma za benki hiyo wakati wa Kongamano la kibiashara lililoandaliwa na Benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wadogo na wa kati mkoani Dodoma lilillofanyika hivi karibuni jijini humo.


Maofisa waandamizi wa Benki ya NBC wakichangia mada kwenye kongamano hilo.
Maofisa waandamizi wa Benki ya NBC wakichangia mada kwenye kongamano hilo.
Maofisa waandamizi wa Benki ya NBC wakichangia mada kwenye kongamano hilo.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC wakichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC wakichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC wakichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC wakichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Muwakilishi kutoka Baraza la Uwezeshaji (NEEC) Bi Nyakao Mturi akiwasilisha mada wakati wa Kongamano hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...