Na Zainab Nyamka, globu ya Jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu  imewaondolea mashtaka mawili ya utakatishaji,  kati ya kumi yaliyokuwa yakiwakabili aliyekuwa rais wa club ya Simba Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange Kaburu baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka hayo dhidi yao.

Hata hivyo, washtakiwa hao pamoja na aliyekua ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Zacharias Hansppope wamekutwa na kesi ya kujibu katika mashtaka saba ambayo ni kughushi, kula njama, matumizi mabaya ya madaraka, kutoa nyaraka za uongo, na kutoa maelezo ya uongo ambayo upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa

Kufuatia kuondolewa kwa shtaka hayo ya utakatishaji  washtakiwa wamepatiwa masharti ya dhamana kwa sababu mashitaka ya utakatishaji fedha ambayo yaliwanyima dhamana hayapo

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Akisoma uamuzi huo, hakimu Simba  amesema ni jukumu la upande wa mashtaka kuthibitisha mashtaka yote kwa washitakiwa na kila shtaka linatakiwa kuthibitishwa peke take na sio kwa kutegemeana.

 "Baada ya kuchambua ushahidi wa mashahidi 10 wa upande wa mashitaka, ukiacha shtaka la tano na sita mahakama imeona kuwa washtakiwa wanakesi ya kujibu katika shtaka la 1,2,3,4,7,8 na 9  isipokuwa katika shitaka la tano na sita na  ambayo shtaka la utakatishaji linaondolewa" amesema hakimu Simba.

Kufuatia kuondolewa kwa mashtaka hayo, Wakili wa washtakiwa hao Nehwmia Nkoko aliiomba mahakama kuwapatia wateja wake dhamana kwani mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo yaliyokuwa yanawanyima dhamana washitakiwa hayapo.

Wakili wa Takukuru, Leornad Swai alipoulizwa kama ana pingamizi lolote juu ya dhamana alidai hawana pingamizi ambapo Hakimu Simba aliwapatia masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini 2 watakaosaini bondi ya Sh.Mil 30 kwa kila mmoja pamoja na kuwa na vitambulisho

Kesi hiyo imeahirishwa hadi leo Septemba 20, 2019 kwa ajili ya washitakiwa kuanza kujitetea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...