VIONGOZI tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ikiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi  wamekutwa na kesi ya kujibu na wataanza kujitetea wiki ijayo kwa siku tatu mfululizo. Septemba 17,18,19 mwaka 2019

Hatua hiyo imefikwa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya upande wa mashtaka kufunga kesi yao kwa kuita mashahidi nane

 Mbali ya Mbowe washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu Taifa, Dk Vincent Mashinji ,  Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika,  Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji na Mbunge wa Kawe  Halima Mdee.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

habari kamili itafuata hivi punde.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...