Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
WAKALA wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) watoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa Halmashauri ya Chalinze wapewa mafunzo kwaajili ya kujipatia leseni kwa njia ya mtandao.

Akizungumza na waaandishi wa habari Afisa Biashara mwandamizi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Boniface Mrema amesema kuwa wafanyabiashara wa halmashauri ya Chalinze wamepewa mafunzo wezeshi kwaajili ya kupata leseni mpya au kurudia kusajili leseni zao za biashara.

"Wafanyabiashara wa halmashauri ya Chalinze wamepewa mafunzo na maafisa wa kutoka Wakala ya Usajili biashara na Leseni (BRELA) ili waweze kupata leseni za biashara zao kwa njia ya mtandao na kuachana na namna ya zamani ambayo ilikuwa ikiwapotezea muda wa kufanya biashara zao". Amesema Mrema.

Nae Afisa Leseni Mwandamizi wa BRELA, Abas Kothema amesema kuwa Tanzania ya Viwanda lazima iwe na mfumo sahihi wa kusajili biashara kwa njia ya mtandao kwani mataifa mengi duniani husajili biashara kwa njia ya mtandao.

Pia amewaasa wafanyabiasha wa Manispaa zilizochaguliwa kwaajili ya kupewa mafunzo wachukue fursa hiyo kwaajili ya kujipatia leseni zao kwa njia ya mtandao na kutokupoteza muda.

Hata hivyo Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa halmashauri ya Chalinze, Lawrence Tsingay ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwachagua wafanyabiashara wa Chalinze kuwa wamojawapo kati ya halmashauri zilizochaguliwa kupewa mafunzo ya kujisajili na kujipatia leseni kwa njia ya Mtandao.

Nae Mfanyabiashara Farida Khamis amewashukuru maafisa BRELA kwa kazi wanayoifanya na kuwaelimisha wafanyabiashara wa Chalinze kwani wamewapunguzia muda wa kupanga foleni walipokuwa wakitafuta leseni za biashara zao.
Afisa Leseni Mwandamizi wa BRELA, Abas Kothema akizungumza na wafanyabiashara wa  Manispaa ya Chalinze kwaajili ya kuwajengea uwezo waweze kujipatia Leseni za Biashara kwa njia ya mtandao.

Afisa biashara Mwandamizi kutoka Wizara ya Biashara na Viwanda, Boniface Mrema akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa Halmashauri ya Chalinze ambayo yanahusu wafanyabiashara kujipatia Leseni kwa njia ya Mtandao baada ya kuzinduliwa Mwanzoni mwa Oktoba,2019.


Baadhi ya wafanyaiashara wa  Halmashauri ya Chalinze wakisikiliza mafunzo yanayotolewa na BRELA kwaajili ya kuwarahisishia wafanyabiashara hao kujipatia Leseni kwa njia ya Mtandao.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara  Halmashauri ya Chalinze, Lawrence Tsingay akizungumza mara baada ya kupewa mafunzo kwaajili ya kuijipatia Leseni kwa njia ya Mtandao katika mafunzo yaliyofanyika Chalinze leo.
Mfanyabiashara  wa Halmashauri ya Chalinze, Farida Khamis akizungumza mara baada ya kupewa mafunzo ya kujisajiri na kujipatia Leseni kwa njia ya mtandao. Amesema kuwa Mafunzo hayo yamekuja kwa muda muafaka kwani itawarahisishia kujipatia leseni bila kupanga foleni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...