Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi ambao ni wachezaji wa mpira wa kikapu (BasketBall) wa Shule ya Sekondari ya Orkeeswa jana Wilayani Monduli Jijini Arusha. 
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Orkeeswa iliyopo Wilaya ya Monduli Jijini Arusha alipowatembelea jana , ambapo alipata fursa ya kuona vipaji vya michezo mbalimbali inayofanywa na wanafunzi hao.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Mwenye kofia) akipata maelekezo kuhusu wachezaji wa mpira wa kikapu (hawapo katika picha) kutoka kwa Mkurungezi wa Shule ya Sekondari ya Orkeeswa Bwana Peter Luis (kulia) alipoitembelea jana Wilaya ya Monduli Jijini Arusha pembeni ya Waziri ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bwana Robert Siyantemi.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiangalia vikombe mbalimbali walivyoshinda wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Orkeeswa katika mashindano waliyowahi kushiriki ndani na nje ya nchi.

(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...