Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuhakikisha wanazuia uhalifu na kulinda usalama wa raia, Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limeendesha msako na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 72 wa makosa mbalimbali.

Watuhumiwa waliokamatwa ni wahalifu wasiofuata sheria katika biashara ya mafuta ya Petroli na Diesel ambao wamekua wakisafirisha katika njia hatarishi kwenye magari ya abiria huku wengine wakikamatwa na nyara za Serikali pamoja na Dawa za kulevya.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo, Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Giles Muroto amesema wao kama chombo kinachohusika na ulinzi wa raia na mali zake pamoja na usalama hawatokubali kuruhusu uhalifu wowote ndani ya Dodoma.

Kamanda Muroto amesema kitendo cha Madereva kusafirisha mafuta kwenye gari za abiria kinaweza kusababisha maafa makubwa endapo yatalipuka.

" Sheria inakataza kabisa kusafirisha mafuta kwa kutumia vyombo vya usafiri wa abiria, hawa wanaweka madumu ya Petroli kwenye buti halafu hizi gari zinafanya safari ndefu msuguano ukitokea tu moto unalipuka.

" Tumekamata magari takribani sita ya abiria yanayosafirisha mafuta haya yote kwa ujumla wao yanabeba abiria siyo chini ya 200, hatuwezi kukubali maafa yawapate Wananchi wetu kwa tamaa za hao madereva, hivyo tumewakamata na tutawachukulia hatua," Amesema Kamanda Muroto.

Amesema Jeshi hilo pia limekamata mtuhumiwa Jonathan Temu (41) mkazi wa Dodoma akiwa na nyama ya wanyamapori aina ya Nsya wanne, Digidigi mmoja aliyoipata kutokana na uwindaji haramu

Kamanda Muroto amesema uchunguzi zaidi unaendelea ili kuipata silaha aliyokua anaitumia kwenye uwindaji huo sambamba na washiriki wengine na mara uchunguzi utakapokamilika atapandishwa mahakamani.

Msako huo pia uliwakamata wanawake watatu wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili yao, pamoja na watuhumiwa wengine waliokutwa na Dawa za Kulevya aina ya Bangi, Mirungi na mitambo ya kutengeneza pombe haramu ya Gongo.

Kamanda Muroto ametoa onyo kwa wote wanaovunja Katiba ya Nchi kwa kufanya mambo ambayo ni kinyume na sheria na taratibu huku akiapa kuwashughulikia wahalifu wote ndani ya Mkoa wa Dodoma.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Dodoma leo
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto akionesha gari lililobeba madumu ya mafuta aina ya Petroli na Diesel kinyume na Sheria jambo ambalo linahatarisha usalama wa abiria
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto akionesha pikipiki walizozikamata ambazo zimekua zikihusika na uhalifu sehemu mbalimbali za Mkoa wa Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...