JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja aitwaye WILLIAM MWAZEMBE [45] Mkazi wa Kijiji cha Ikukwa akiwa na bhangi gramu 300.
Mtuhumiwa alikamatwa tarehe 17 Septemba, 2019 saa 19:30 usiku huko eneo la Chunya mjini, Kata ya Itewe, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya katika msako mkali uliofanyika maeneo hayo. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi. Upelelezi unaendelea.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja aitwaye BAHATI NDELE, [28] Mkazi wa Ilemi akiwa na bhangi kilogram moja [01] na gramu 210.
Mtuhumiwa alikamatwa katika msako uliofanyika tarehe 17 Septemba, 2019 saa 15:30 alasiri huko eneo na Kata Ilemi, Tarafa Sisimba, Jiji la Mbeya. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi. Upelelezi unaendelea.
Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

 

KUJARIBU KUJIUA KWA KUNYWA SUMU.

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mwanamke mmoja aitwaye SILVIA SANDE [28] Mkazi wa Nsongwi kwa mauaji ya mtoto wake mwenyewe aitwaye ASIFIWE RASHIDI BAINI mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili na kwa jaribio la kujiua yeye mwenyewe kwa kunywa sumu ya kuulia wadudu.

Ni kwamba mnamo tarehe 16 Septemba, 2019 saa 10:00 asubuhi huko Kijiji cha Nsongwi Juu kilichopo Kata ya Ijombe, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya, mtuhumiwa alikunywa sumu ya kuulia wadudu chumbani kwake kwa lengo la kujiua kisha kumnywesha sumu hiyo mtoto wake aitwaye ASIFIWE RASHIDI BAINI mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili, mkazi wa Nsongwi juu.
Mtuhumiwa na mtoto wake baada ya tukio hilo walikimbizwa kituo cha afya Igawilo ambapo mtoto alifariki. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi na mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa Mahakamani. Chanzo cha tukio kinachunguzwa. 
KUPATIKANA NA NISHATI YA MAFUTA BILA KIBALI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa tisa [09] kwa tuhuma za kupatikana na kufanya biashara ya nishati ya mafuta aina ya Diesel na Petrol bila kibali.
Watuhumiwa wamekamatwa katika msako mkali uliofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya tarehe 17 Septemba, 2019 katika maeneo ya Maghorofani, Uyole Jijini Mbeya, Chimala, Igawa na Igurusi Wilayani Mbarali na maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kyela.
Katika msako huo jumla ya lita 1,500 za Petrol na lita 2,500 za Diesel zimekamatwa. Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
  1. MAJALIWA EDWARD [30] Mkazi wa Mwambene
  2. EDSON KALINGA @ MANGI [32] Mkazi wa Iganzo
  3. HAMIS ANYIMIKE [32] Mkazi wa Mafiati
  4. ISSAH MWAMBELO [33] Fundi Magari na Mkazi wa Sae
  5. KAMBELA HAMAD MWIPOPO [30] Mkazi wa Makunguru
  6. GEORGE MWAKALOBO @ MWADADA [40] Mkazi wa Ipinda
  7. MAJUTO SIMONI [37] Mkazi wa Kapwili
  8. LWITIKO MWAIPOPO [38] Mkazi wa Ipinda
  9. JAKOBO MWAKILEMA [47] Mkazi wa Ipinda
Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Imetolewa na:
 [ULRICH OMATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...