· Vodacom yatoa taarifa ya ongezeko la faida kwa mwaka kufikia TZS billioni 90.2


 Kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania, Vodacom Tanzania PLC imetangaza faida ya mwisho wa mwaka ya kiasi cha TZS bilioni 90.2 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ulioishia mwezi Machi mwaka huu.

Wakati huo huo Kampuni ya Vodacom ambayo ina mtandao wenye kasi zaidi nchini inajivunia thamani iliyojitengenezea katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni ikiwemo TZS bilioni 54.5 ambazo zimelipwa kama gawio kwa wanahisa.

Ongezeko hili limechangiwa na kuongezeka kwa mapato yatokanayo na huduma ambayo yanafikia TZS bilioni 1018.9, ambayo yamesababishwa na kukua na kuimarika kwa mapato yatokanayo na huduma za M-pesa, ununuzi wa Intaneti (Bando) na mapato yatokanayo na ujumbe wa simu. Kampuni ya Vodacom imepata wateja wapya wapatao milioni 1.2 katika mwaka huu wa fedha jambo ambalo linaongeza idadi yake ya wateja kufikia milioni 14.1.

Katika mwaka huu wa fedha kampuni ya Vodacom ilifanya uwekezaji mkubwa wa zaidi ya TZS bilioni 171.4 sawa na (asilimia 16.7% ya Mapato) katika kupanua mtandao wake, kuongeza maeneo yanayopata mtandao wa 4G katika miji mikubwa nchini, kuongeza uwezo na kuboresha mtandao kuweza kutoa huduma ya data ya kiwango cha juu kwa wateja.

Wakati huo Shilingi bilioni 59 zimewekezwa katika mishahara, mafunzo na maendeleo ya wafanyakazi wake wa kudumu wapatao 548 pamoja na kutoa ajira isiyo ya moja kwa moja kwa zaidi ya Watanzania 127,000.

Akiongea katika mkutano mkuu wa mwaka wa kampuni ya Vodacom leo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Vodacom bwana Ali A. Mufuruki amesema, “Kampuni ya Vodacom vile vile inajivunia uwekezaji wake katika jamii ambao una thamani ya jumla ya shilingi trilioni 1.1, ambazo ni fedha zilizochangiwa katika uwezeshaji wa jamii kupitia kodi, ada za udhibiti katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ambapo malipo ya zaidi ya Shilingi trilioni 0.4 yalifanyika katika mwaka 2019 peke yake.”

“Ukuaji katika sekta ya mawasiliano imekuwa wa pole pole katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. Tukiwa kama watendaji muhimu katika sekta hii, tunajivunia kuwa chanya katika ukuaji wa sekta hii,” alihitimisha bwana Mfuruki. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...