Na Mwandishi Wetu, Globu ya jamii
KAYA 970 zilizopo katika mtaa wa Kiziza na Nyakale Kata ya kibada wilayani kigamboni jijini Dar es Salaam zimeungana kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya maji kujaa katika makazi yao kwa kutengeneza mtaro wa kupitisha maji pindi mvua zinaponyesha ili kunusuru makazi yao.

Ili kukamilisha mradi wa uchimbaji wa mtaro uliowashirikisha wananchi kujenga hadi kukamilika kwake zinatarajia kutumika kwa shilingi  ya Bilioni moja au Bilioni 1.2.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea baadhi ya mitaro katika eneo la kiziza na nyakale kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mtaro ulipofikia,Mwenyekiti wa mradi wa mitaro kata ya Kibada, Nazzar Nicholaus alisema ulianza kutengenezwa januari 2018 na kasi ya ujenzi unaenda vizuri.

Nicholas ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya wananchi kwa Rais Magufuli,alisema ilikukamilisha mradi wote wa ujenzi wa mtaro wananchi wamekubaliana kushirikiana kwa kujitolea fedha,vifaa na Nguvu kazi.

"Ili kufanikisha mradi huu tunahitaji mkono mrefu na mkono mrefu tunazungumzia serikali.Hata hivyo wananchi tumeamua kuunga mkono juhudi za serikali za kutatua kero za wananchi chini ya Rais mpendwa Dk.John Magufuli kwa kuanza kuitatua kero hii," aliongeza

"Wakati wa kipindi cha mvua ndipo wananchi wa maeneo haya wanakuwa katika wakati mgumu Kutokana na maji kutuama katika makazi yetu hali inayofikia wanafunzi kushindwa kwenda shule na wafanyakazi kushindwa kwenda kwenye majukumu yao hivyo kwa umoja wetu tumeamua kutatua kero hii," alisema Nicholas

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kibada,Amin Sambo alisema mradi huo ulianza mwaka 2005 chini ya wizara ya Ardhi ambapo wananchi wa eneo hilo walipoona mradi huo umesimama ndipo walipoamua kushirikiana kwa pamoja na kuamua kutengeneza moja ya Mtaro mkubwa ambao utapitisha maji kiurahisi n miitado midogo kuunganishwa kwa mtaro huo mkubwa.

"Tunautengeneza mtaro huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, tumeamua kuchangishana na kutengeneza mtaro huo nia yetu ni kumsaidia Rais Magufuli kwa kutumia rasiliamari zetu wenyewe tulizonazo," alisema na kuongeza

"Tayari kazi imeanza na hadi sasa kuna kampuni moja ijulikanayo kwa jina la Plasisco imejitolea kutupatia Makaravati mawili ambayo yatatandikwa katika mtaro huo," amesema.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Mtaa WA Kiziza kata ya Kibada ,Adinani Simba amesema tatizo la maji katika eneo hilo lilianza siku nyingi mvua zinaponyesha na kuathiri nyumba nyingi na watu kushodwa kutoka kwenda kufanya shughuli zao.

Ame1sema katika eneo hilo 1kuna mitaro kama minne ambayo inahitajika kutengenezwa lakini 1wananchi wa eneo hilo wameamua kushirikiana na kutengeza mtaro mmoja mkubwa utakaopitisha maji kutoka katika mtaro mingine.
Kazi ya kuchimba mtaro ikiendelea katika Kata ya Kibada wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam ili kunusuru kaya 970 ambazo zimekuwa na changamoto ya maji kujaa wakati wa mvua za masika
Sehemu ya mtaro huo unaoendelea kuchimbwa kwa nguvu za wananchi wa Kata ya Kibada wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Mradi wa kuchimba Mtaro Kibada wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam, Nizzar Nicholaus akizungumzia kasi ya ujenzi wa mtaro huo unaojengwa kea lengo la kunusuru makazi ya wananchi wa eneo hilo.
Ofisa Mtendaji Kata ya Kibada, Salome Ngonyani akizungumza baada ya ziara ya kukagua mtaro unaochimbwa na wananchi wa Kata hiyo kwa ajili ya kunusuru makazi yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...