Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Tellack akisisitiza jambo wakati akiongea na Wananchi wa Shinyanga katika mji wa Kahama ikiwa ni siku ya kufunga kwa Kampeni ya Kitaifa ya ” USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” iliyofanyika katika viwanja vya Majengo, Kahama.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akieleza jambo wakati akiongea na Wananchi wa Shinyanga katika mji wa Kahama ikiwa ni siku ya kufunga kwa Kampeni ya Kitaifa ya ” USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” iliyofanyika katika viwanja vya Majengo, Kahama.
Mratibu wa kampeni ya ” USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” akitoa salamu za Wizara ya Afya mbele ya Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa ya Shinyanga Mhe Zainab Tellack, wakati wa kufunga Kampeni hiyo katika mikoa ya kanda ya ziwa, tukio limefanyika katika viwanja vya Majengo, Kahama Shinyanga.
Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Tellack wakati wa kufunga kwa Kampeni ya Kitaifa ya ” USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” iliyofanyika katika viwanja vya Majengo, Kahama.
Umati wa watu uliojitokeza kumsikiliza mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Tellack wakati wa kufunga Kampeni ya Kitaifa ya ” USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” iliyofanyika katika viwanja vya Majengo, Kahama.
***********************************

Na Rayson Mwaisemba WAMJW-SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Tellack amewaasa Wananchi wa Mkoa huo kujikita katika huduma za kukinga kuliko kutibu magonjwa ili kuondokana na gharama kubwa zinazotumika katika kutibu kwenye ngazi ya familia na Serikali.

Wito huo ameutoa wakati akiongea na Wananchi wa Shinyanga katika mji wa Kahama ikiwa ni siku ya kufunga kwa Kampeni ya Kitaifa ya ujenzi wa vyoo bora na kuvitumia kwa usahihi ” USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” iliyofanyika katika viwanja vya Majengo, Kahama.

Mhe. Zainab Tellack amesema kuwa idadi kuwa ya magonjwa ya mlipuko nchini kama vile kuhara na kipindupindu yanatokana na tatizo la kutokuwa na vyoo bora na kutonawa mikono kwa maji safi chirizika na sabuni hali inayopelekea kuingia gharama kubwa kutibu magonwa hayo.

“kuna maradhi mbali mbali ambayo Watanzania wanayapata, ambayo si ya lazima, maradhi kama Kipindupindu, Kuhara, Minyoo ambayo yanasababishwa na ukosefu wa vyoo, na kuvitumia kwa usahihi, huku wengine wakitoka vyooni hawanawi mikono matokeo yake wanakula kinyesi jambo linalopelekea kupata magonjwa ambayo yanawagharimu katika matibabu” Alisema Mhe. Zainab Tellack.

Aliendelea kutoa wito kwa kusisitiza, ujenzi wa choo bora na matumizi sahihi utasaidia kupunguza matumizi ya dawa mara kwa mara ambayo hayana ulazima, jambo litalosaidia kupunguza usugu dawa, na madhara mengine madogo madogo yatokanayo na matumizi ya dawa.

Aidha, Mhe. Zainab Tellack ameahidi kuwa, kama Mkoa ifikapo Disemba 31 kaya zote katika Mkoa wa Shinya lazima zitakuwa na vyoo bora, na kuvitumia vyoo hivyo kwa usahihi ili kuendelea kujikinga dhidi ya magonjwa ya Kipindu pindu, kuhara na minyoo.

“Ndugu zangu Wanakahama na Shinyanga kwa ujumla sisi kama Mkoa tumeahidi, kwamba ifikapo Disemba 31, kaya zetu zote kwenye Mkoa huu lazima ziwe na vyoo, hilo ndugu zangu tunaweza, kama vijana wetu wanathamani kubwa kwanini tushindwe kujenga vyoo” alisema Mhe. Zainab Tellack.

Katika Mkutano huo, Mhe. Zainab Tellack alikubaliana na Wananchi wa Mkoa huo kuwa ifikapo Disemba 31 kwa Wananchi wataokuwa hawana vyoo watapigwa faini ya kiasi cha shilingi 500,000 na kuchukuliwa hatua kali dhidi yao.

“Ambae hatokuwa na Choo bora ifikapo Disemba 31, faini 500,000 tumekubaliana hivyo, na mmesema wenyewe, na mimi nabariki hilo, kwa hiyo tujipange ili tusifike huko” Mhe. Zainab Tellack.

Kwa upande wake Mratibu wa Kampeni ya “USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” Bw. Anyitike Mwakitalima amesema kuwa kila dakika moja Dunia inapoteza watu 4, sawa na watu 6000 kila siku, huku sababu ya vifo hivyo ikiwa kula kinyesi hali inayotokana na kutotumia vyoo na kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni, huku wahanga wakubwa wa tatizo hili wakiwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

“Kila dakika moja Dunia inapoteza watu 4, ikiwa inamaana kwamba kila siku Dunia inapoteza watu 6000, na hawa ni kwasababu tu wamekula kinyesi na wengi wao ni Watoto wenye umri chini ya miaka mitano” alisema Bw. Anyitike Mwakitalima

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...