Balozi Ramadhan Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mara yanayondelea mjini Mugumu, Wilayani Serengeti. Kongamano hili linalojumuisha wadau kutoka Tanzania na Kenya, linalenga kujadili mustakabali wa bonde la Mto Mara na nafasi yake katika shughuli za uhifadhi.

Akizungumza katika kongamano hilo Balozi Mwinyi amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Kenya katika shughuli zote zinazolenga kujenga ustawi wa uchumi na jamii, na kuendeleza uhusiano imara uliopo baina ya nchi hizi mbili bila kusahau suala la uhifadhi wa mazingira ya bonde la Mto Mara.

Aidha amewataka wadau kuwa huru kutoa mawazo yao yanaoyelenga kutatua changamoto za uhifadhi zinazolikabiri bonde hilo sambamba na kuboresha jitihada na mikakati inayotumika sasa.Kongamano hili linatarajiwa kutoa maazimio ambayo yatatoa uelekeo mpya na kuongeza kasi ya utekelezaji wa shughuli na jitihada za uhifadhi wa Bonde la Mto Mara.

Tarehe 15 Septemba, 2019 inatarajiwa kuwa siku ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mara yanayoendelea kufanyika mjini Mugumu wilayani Serengeti. 
Meza kuu ikifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea wakati wa kongomano la Siku ya Mara lililofanyika katika ukumbi wa Kisarare mjini Mugumu, Serengeti 
Balozi Ramadhan Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,akifuatilia jambo wakati kongamano likiendelea 
Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara, ambaye pia alikuwa mgeni wa heshima katika kongamano hilo akizungumza na hadhira iliyojitokeza (hawapo pichani) kujadili changamoto za uhifadhi wa Bonde la Mto Mara 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...