Mafunzo kwa njia ya mtandao (ECHO Project) katika Sekta ya Afya yametajwa kuwa na manufaa makubwa nchini kwani hivi sasa wataalamu wengi wanafikiwa na kupewa mafunzo mbalimbali kwa mara moja kuliko hapo awali.

Hayo yameelezwa leo Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Uchunguzi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Alex Magesa alipokuwa akifungua mafunzo maalum kwa wataalamu wapatao 110 wa sekta ya afya yaliyolenga kuwajengea uwezo zaidi juu ya mfumo huo.

Amesema kupitia mafunzo hayo Serikali imeweza kuokoa gharama za kusafirisha wataalamu wengi kwenda mafunzo, ambapo kupitia program hiyo sasa hutumia wastani wa Sh bilioni 14 kwa mafunzo ya wataalam wapatao 20 hadi 30 kwa mara moja.

Amesema kwa taratibu walizoweka, wamekuwa na dhima ya kutekeleza agizo la Serikali ambapo Rais, Dk. John Magufuli aliwataka kuhakikisha wanaweza kupunguza gharama za uendeshaji wa mafunzo.

Mratibu wa Mradi wa ECHO, Jacob Lusekelo amesema ulianza rasmi kutumika nchini tangu 2016.
“Tanzania ni nchi ya kwanza kusimika mfumo huo barani afrika ni mzuri kwani unasaidia kupunguza sana matumizi ya gharama ambazo tumekuwa tukizitumia kusafiri sehemu moja hadi nyingine kupashana habari za masuala mbalimbali muhimu kwa tiba,” amesema.

Daktari Abuu Maghimbi kutoka Chuo Kikuu cha Maryland amesema wanashirikiana kwa ukaribu na Serikali katika uendeshaji wa mfumo huo na kwamba hadi kufikia 2020 wanakusudia kuvifikia vituo 200.
 Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Uchunguzi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Alex Magesa (kulia) akisoma hotuba alipokuwa akifungua mafunzo maalum ya (ECHO Project)   kwa wataalamu wapatao 110 wa sekta ya afya yaliyolenga kuwajengea uwezo leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza  Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Uchunguzi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Alex Magesa wakati wa akifungua mafunzo maalum ya (ECHO Project) (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...