Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv,

MWANASIASA Salma Mntambo, amehukumiwa kifungo cha miaka 99 jela  baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka  17 yaliyokuwa yakimkabili yakiwemo ya kuwasilisha nyaraka za uongo na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hukumu hiyo imesomwa leo Septemba 18,mwak 2019 na  Hakimu Mfawidhi Kelvin Mhina Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mhina amesema, Mahakama kupitia mashahidi watano waliolioletwa na upande wa mashtaka wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo.

 "Nimepitia sababu za upande wa mashtaka na utetezi katika kesi hii na ninamuhukumu mshtakiwa kuwa, katika makosa matatu ya kutoa nyaraka za uongo atatumikia kifungo cha miaka mitano jela kwa kila kosa na pia katika makosa 14 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka sita jela kwa kila kosa,"amesema hakimu Mhina.

Hata hivyo Hakimu Mhina amesema adhabu hizo zitaenda pamoja hivyo mshtakiwa  atakaa gerezani kwa miaka sita tu. Pia Mahakama imesema kuhusu suala la fidia atatafakari na kufanya utafiti ili aje kutoa oda ambayo ni sahihi hivyo Oktoba 2, mwaka huu atatoa oda hiyo ya fidia


Katika kesi hiyo, mshtakiwa huyo alikuwa akikabiliwa na mashtaka 24 hata hivyo ametiwa hatiani katika mashtaka 17 yakiwamo ya kutakatisha fedha jumla ya Sh. 1.027,000,000 kutoka kwa Ridhuan Mringo huku akijua fedha hizo zimetokana na zao la makosa tangulizi ya kugushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuwasilisha nyaraka za uongo. 

Katika kosa la kugushi,  mshtakiwa Mntambo anadaiwa kati ya June mosi 2003 na Oktoba 31, mwaka 2011 maeneo yasiyojulikana Wilayani Ilala, mkoani Dar es Salaam kwa nia ya udanganyifu aligushi risiti yenye namba 001226 ya tarehe 10/06/2003 ili kuonesha kwamba Ridhuan Mringo alinunua nyumba ya Shirika la Nyumba iliyopo Plot namba 710 mtaa wa Mfaume Upanga kwa Sh. Millioni 70 wakati akijua ni uongo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...