Wakati mkutano mkuu wa 21 wa mwaka wa wakuu wa polisi wa nchi za ukanda wa mashariki mwa Afrika (EAPCCO)ukitarajiwa kufanyika wiki hii jijini Arusha, imeelezwa kuwa bado kuna matishio ya kiusalama ambapo magenge ya uhalifu bado yameendelea kusumbua katika ukanda huo yakiwemo vitendo vya ugaidi na mafunzo ya kihafidhina.

Hayo yamebainishwa jijini Arusha na mkuu wa jeshi la polisi nchini Simon Sirro wakati akifungua kikao cha siku mbili cha kamati tendaji za EAPCCO kitakachofuatiwa na mkutano mkuu wa 21 wa mwaka wa wakuu wa polisi kutoka katika nchi 14 wanachama wa shirikisho hilo ambapo wajumbe hao ambao ni wataalamu wa masuala ya upelelezi,sheria,mafunzo,kuzuia vitendo vya kigaidi na jinsia wanategemewa kuja na matokeo chanya yatakayojenga agenda za mkutano huo wa 21. 

IGP Siro amesema matukio ya kigaidi yanayotokea maeneo mbalimbali duniani ni kiashiria tosha kwamba na nchi za ukanda huo pia hazipo salama.

Awali kamisha mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini Robert Boaz amesema katika mkutano huo wa siku mbili wajumbe wa kamati hizo watapata fursa ya kujadili mbinu mbalimbali za mikakati ya kukabiliana na uhalifu ambapo mkuu wa sekretarieti ya RB Nairobi Gidion Kimilu amesema bara la afrika linashuhudia kuibuka kwa uhalifu mpya wa kimtandao unaoletwa na teknlogia haswa kwa vijana ambao asilimia kubwa hawana ajira

Tangu kuanzishwa kwa shirikisho la wakuu wa polisi wa nchi za mashariki mwa afrika agenda kuu imekuwa ni Kuimarisha usalama,Amani na utulivu kwa raia na mali miongoni mwa nchi washirika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...