Mradi wa Uboreshaji wa Reli ya Kati – TIRP Dar es Salaam – Isaka wafikia 40% tangu kuanza utekelezaji wake mwezi Juni 2018
Mashine zinazotumika katika uboreshaji wa reli hiyo zikiendelea na kazi kwenye la reli Kati ya – TIRP Dar es Salaam – Isaka ambapo umefikia asilimia 40% tangu kuanza utekelezaji wake mwezi Juni 2018

Mradi wa Uboreshaji wa Reli ya Kati – TIRP Dar es Salaam – Isaka wafikia 40% tangu kuanza utekelezaji wake mwezi Juni 2018. Mradi huo unahusisha uboreshaji wa miundombinu ya reli ikiwemo Makalavati, tuta la reli, Madaraja makubwa na madogo na kuweka mifumo ya kisasa ya mawasiliano na uendeshaji wa treni kuanzia Dar es Salaam hadi Isaka urefu wa Kilometa 970.

Lengo la mradi wa Uboreshaji wa Reli ya Kati ( TIRP) ni kuiwezesha reli ya zamani (Meter Gauge) kutoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo kwa ufanisi na uhakika kutokana na uchakavu wa miundombinu ya reli ya ‘Meter Gauge’ yenye umri wa zaidi ya miaka mia moja (100) tangu ilipojengwa wakati wa ukoloni.

Kazi inayofanyika ni kuimarisha tuta kwa kuondoa kokoto za zamani na kuweka kokoto mpya, kuimarisha Makalavati, Madaraja makubwa na madogo, lakini pia wahandisi wanaendelea na kazi kubwa ya kuiunganisha reli Dar es Salaam – Isaka kwa kutumia mashine ya ‘Mobile Flash Butt plant’ na kuifanya reli kuwa moja (contionus welded rail), mashine hiyo ina uwezo wa kuzalisha joto kali lenye uwezo wa kuunga vipande viwili vya reli kwa muda wa sekunde 120.

Kutumika kwa teknolojia hii mpya ya kuunganisha reli itqsaidia treni za abiria na mizigo kwenda mwendokasi hadi Kilometa 75 kwa saa tofauti na hapo awali ambapo treni zilikuwa zikienda Kilometa 30-35 kwa saa, hii itasaidia kupunguza muda wa safari na kusaidia kuendelea kwa kasi kwa shughuli nyingine za kiuchumi.

Faida nyingine ni kuongezeka kwa uwezo wa treni za mizigo kubeba mzigo mkubwa zaidi.Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu kutoka TRC Mhandisi Maizo Mgedzi ameeleza kwa undani mabadiliko yanayotarajiwa kupatikana mara baada ya mradi huu kukamilika, amesema kuwa mwendokasi wa treni utaongezeka sambamba na uwezo wa kubeba mizigo.

“Tunazirefusha njia za kupishana kwahiyo tutaweza kupitisha treni ya urefu wa Mita 600 badala ya Mita 400, tunaiongezea uwezo reli Dar – Isaka ya uwezo wa kubeba mizigo kutoka tani 14 – 18.5, kutoka mwendokasi wa Kilometa 30 hadi 75 kwa saa, pia abiria akipanda itakuwa raha mustarehe hakutakuwa na kurukaruka kwa sababu reli itakua imeiungwa vizuri kwa kutumia mashine ya umeme,alisema Maizo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...