Sebastian Atilio akiwa katika mahakama ya Wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa kabla ya kusomewa mashtaka yake leo mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo.

MWANDISHI wa habari wa kujitegemea anayeandika habari zake katika ukurasa wa kitabu sura (face Book )katika wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa Sebastian Atilio amefikishwa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Mufindi kwa makosa mawili likiwemo la kuandika habari za uongo na kufanya kazi bila kusajiliwa na bodi anaripoti mwandishi Francis Godwin kutoka mkoani Iringa.

Akisoma mashtaka haya leo mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Edward Uforo .mwendesha mashitaka wa jamhuri Victor Kitamale alisema kuwa Sebastian anashitakiwa kwa kosa la kwanza kufanya kazi bila kusajiliwa katika bodi ya uandishi na kosa la pili ni kuandika habari za uongo juu ya wananchi wa kijiji cha Ifupila kuhamishwa .

Hata hivyo msitakiwa huyo alikana mashitaka yote yanayomkabili huku mahakama hiyo ikisema kuwa makosa hayo kisheria yanadhamana .

Wakati mwendesha mashtaka wa jamhuri alipinga dhamana hiyo chini ya kifungu namba 148(5) D) cha sheria na mwenendo wa makosa ya jinai (sura 20) ambapo jamhuri imefaili kiapo cha kuzuia dhamana kutolewa.

Huku upande wa mashtaka umepewa na mahakama hiyo nafasi ya kufaili hati kinzani Septemba 16 mwaka huu ili Septemba 18 mwaka huu maombi ya kutolewa ama kutotolewa kwa dhamana yatajulikana.

Wakili wa mwanahabari huyo Emmanuel Chengula kutoka mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC) alisema kuwa hatua ya kufikishwa mahakamani kwa mteja wake ni mwanzo wa haki yake kupatikana kwani polisi walikuwa wakimzuia mahabusu mteja wao toka jumamosi iliyopita bila kumpeleka mahakamani.

Wakili Chengula alisema katika kesi hiyo kuna maombi ya kuzuia dhamana ambayo ni maombi namba 10/2019 na kesi yenyewe ya msingi ni kesi namba 208/2019.

Mshitakiwa huyo amepelekwa katika mahabusu ya Isupilo Mufindi hadi septemba 18 atakapofikishwa mahakamani hapo tena kwa ajili ya kusikiliza maamuzi ya dhamana yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...