Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MWILI wa aliyekuwa mwandishi wa habari mkongwe nchini Gofrey Dilunga aliyefariki dunia Septemba 17 mwaka 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili umeagwa leo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea mjini Morogoro ambapo utapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Serikali haitasahau mchango wa marehemu Dilunga hasa katika kuitumia vyema kalamu yake kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.

Dkt. Mwakyembe amesema kutokana na mchango wake mkubwa katika taifa Rais Dkt. John Joseph Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani na waziri Mkuu Kassimu Majaliwa wametuma salamu zao za rambirambi kwa ndugu, jamaa, marafiki na wanahabari wote.

" Kuna vikao vya dharura vinavyoendelea ila nimelazimika kuja hapa kutokana na mchango wake,na kutokana na umuhimu Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wamenituma kuja kutoa salamu zao za rambirambi" ameeleza Dkt. Mwakyembe.

Kwa upande wake Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema kuwa mchango wa marehemu katika taifa na chama hicho ni mkubwa na daima alikuwa mstahimilivu aliyetumia kalamu yake vyema kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.

Amesema kuwa waandishi wa habari hawana budi kufuata nyayo zake ili kuweza kulipeleka taifa mbele zaidi na hiyo ni kwa kutumia vyema kalamu zao.

Akisoma wasifu wa marehemu Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamhuri Deudatus Balile amesema kuwa marehemu alianza kusumbuliwa na maradhi ya tumbo kuanzia julai mwaka huu kabla ya kupelekwa hospitali ya taifa Muhimbili ambapo umauti ulimkuta.

Balile amesema kuwa marehemu ameacha watoto watatu na mjane mmoja na kueleza kuwa kampuni hiyo itamsomesha mtoto wa kwanza wa marehemu hadi elimu ya juu na amewaomba wanajamii wengine kuendelea kuwashika mkono watoto wa marehemu na mjane huyo.

Viongozi mbalimbali wa kisiasa na serikali wamejitokeza kuaga mwili wa mwandishi huyo wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe.

Pia alikuwepo Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas, Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa, na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole.

Wengine ni Mbunge wa Mtama Nape Nnauye, Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, wabunge, viongozi wa taasisi mbalimbali na wanahabari.
Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga leo Septemba 19 katika  viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe akimsalimia Mke wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Jamhuri  Godfrey Dilunga .
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa akimpa mkono wa pole  Mke wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari Godfrey Dilunga katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa kuaga mwili wa Mwandishi huyo.
Mbunge wa Viti Maalum Amina Mollel akizungumza wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga 
Mbunge wa Viti Maalum Amina Mollel akimpa mkono wa pole Mke wa marehemu Godfrey Dilunga akisalimiana na 
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akizungumza wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga .
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe akimuonesha kitu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga ,Kushoto ni Mbunge wa viti maalum Amina Mollel,Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi,na kulia ni Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe na Meya wa Ilala Omari Kumbilamoto.
Sanduku  lililobeba mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari maarufu Godfrey Dilunga likishushwa viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam tayari kwa kuagwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa(kulia) akisalimiana na Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe  baada ya kukutana viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga .Wa kwanza kulia ni Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa(kushoto)akiwa na waombolezaji wengine kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 

Mtangazaji wa Clouds TV  na Clouds Redio Simon Simalenga(kushoto) akizungumza jambo mbele ya waandishi wengine wa wahabari waliofika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 
Sehemu ya waandishi wa habari nchini wakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaa n kuaga mwili wa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga .Kuanzia kushoto ni Jamal Hashim, Emmanuel Mbuguni na Idd Mkwama
Mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Dodfrey Dilunga ukishushwa katika gari baada ya kufika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 
Jeneza la mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Jamhuri Godfrey Dilunga ukishushwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuuga kabla ya kuanza safari ya kuusafirsisha mkoani Morogoro kwa ajili ya maziko yanayotarajia kufanyika kesho
Waombolezaji wakiweka vizuri jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Jamuri marehemu Godrey Dilunga 
Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini wakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa nwandishi wa habari nchini Godfrey Dilunga
Waombolezaji wakiwa wamesimama kwa ajili ya maombi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga
Baadhi ya waombolezaji waliofika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa Godfrey Dilunga wakiwa wamesiamama wakati wa ibada maalum 
Waombolezaji wakiwa wamesimama wakati wa ibada maalum ya kumuombea aliyekuwa mwandishi wa habari maarufu nchini Godfrey Dilunga
Sehemu ya waombolezaji wakiwa wamesimama wakati wa shughuli za kuaga mwili wa mwandishi Godfrey Dilunga katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa wa Kampuni ya Jamhuri inayochapisha gazeti la Jamhuri Deodatus Balile akizungumza wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa gazeti hilo Goddrey Dilunga .Mwii wa marehemu Dilunga umeagwa leo viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam  
Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Mazishi ya aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga, Thomson Kasenyenda akitoa ufafanuzi na maelezo kwa waombolezaji waliofika kuaga mwili wa marehemu Dilunga 
Katibu wa Jukwaa la  Wahariri Tanzania(TEF) Nevill Meena akizungumza mbele ya waombolezaji waliofika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Afrika Group Media inayosimamia kituo cha Luninga cha Chanel Ten na kituo cha Redio cha Magic FM Jaffary Haniu akitoa salamu za pole wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Jamhuri Godfrey Dilunga ambaye ameagwa leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 
Mhariri Mkuu wa Gazeti la Mtanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Jukwaa la Wahariri wa Habari Tanzania (TEF)Kulwa Karedia(kushoto) akizungumza leo Septemba 19,2019 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa mwandishi Godfrey Dilunga 
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania(TAMWA) Joyce Shebe ambaye pia ni Mhariri wa Clouds Redio na Clouds TV akitoa neno wakati wa kuaga mwili wa marehemu Godfrey Dilunga aliyefariki dunia Septemba 17 mwaka huu .Dilunga ameagwa leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 
Baadhi ya waombolezaji wakiwemo viongozi wa Serikali, viongozi wa vyama vya siasa na wadau wa tasnia ya habari wakiwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa mwandishi mkongwe Godfrey Dilunga aliyefariki dunia Septemba 17 mwaka huu.Marehemu Dilunga anatarajiwa kuzikwa kesho mkoani Morogoro
Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akizungumza mbele ya waombolezaji waliofika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari mkongwe nchini Godfrey Dilunga ambaye amefariki dunia Septemba 17, 2019 
Katibu wa Itikadi na Uenezi- CCM Hamphrey Polepole akitoa salamu za pole kwa niaba ya chama hicho wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa habari Godfrey Dilunga aliyeagwa leo  katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe(kulia) akisalimiana na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe 
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam baada ya kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Jamhuri, Godfrey Dilunga 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...