Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
KONGAMANO la tatu la sekta ya mafuta na gesi litakalofanyika Oktoba 2 na 3 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijiji Dar es Salaam litazikutanisha nchi 67 ambazo zitawaweka pamoja wadau na viongozi muhimu wa sekta ya nishati kutoka serikalini na sekta binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Afisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya Ocean Business Partners na mwenyekiti wa jumuiya ya watoa huduma ya nishati ya mafuta na gesi nchini Balozi Abdulsamad Abdulrahim amesema kuwa malengo ya kongamano hilo ni pamoja na kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Joseph Magufuli ambaye daima amekuwa akihamasisha kujenga nchi ya viwanda na kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati.

"Tutaendelea kuunga mkono jitihada za mheshimiwa Rais na kupitia kongamano hili tunategemea kufukua ajira, bunifu mbalimbali pamoja kuweka mahusiano bora ya kibiashara baina ya wazawa na wageni" ameeleza Abdulsamad.

Amesema kuwa kongamano hilo litakalowakutanisha washiriki zaidi ya 600 litachambua umuhimu wa kimkakati na nafasi ya Tanzania kama kitovu cha Afrika Mashariki katika uendelezaji mkubwa wa sekta ya nishati.

"Washiriki wa kongamano hili watapata fursa ya kufahamu hali ya sasa ya sekta ya nishati nchini, mikakati ya kufikia Tanzania ya viwanda pamoja na kujifunza namna ya kufanya makubaliano ya kibiashara baina ya makampuni ya kimataifa na yale yaliyoko nje ya nchi" ameeleza Abdulsamad.

Amesema kuwa mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo mipango ya muda mfupi ya usambazaji na uhitaji wa nishati nchini,  ushiriki wa wajasiriamali wadogo katika sekta hiyo pamoja na ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi katika kuyafikia malengo na hiyo itaenda sambamba na utoaji wa tuzo maalumu kwa baadhi ya washiriki.

" Tuzo mbalimbali zitatolewa ikiwemo tuzo kwa kampuni bora nchini, kampuni bora ya kimataifa na kampuni bora ya mfano ya wazawa pamoja na tuzo nyingine kwa wanafunzi wa vyuo walioshinda katika mashindano ya insha ambao watapata ufadhili wa masomo ili kuendeleza vyema sekta hii na pia mwanamke shupavu katika sekta hiyo na tutawasajili wanawake wote ili kutoa chachu kwa wanawake wengine" ameeleza.

Balozi Abdulsamad amesema kuwa viongozi mbalimbali wa wa Serikali wakiongozwa na waziri wa nishati Dkt. medard Kalemani watashiriki katika kongamano hilo ambalo pia limetoa fursa za kutangaza vivutio vya utalii na kutoa ajira na fursa mbalimbali za kiuchumi kwa watanzania.
Mwenyekiti wa jumuiya ya watoa huduma ya nishati ya mafuta na gesi nchini na Afisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya Ocean Business Partners      Balozi Abdulsamad Abdulrahim na Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kongamano la tatu la sekta ya mafuta na gesi na kueleza kuwa fursa zaidi ajira na uwekezaji zinategemewa kupatikana kupitia kongamano hilo, leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...