Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akionyesha kitabu cha Kanuni za Baraza la Kiswahili la Taifa mara baada ya kuzindua leo Jijini Arusha.

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza jambo mara baada ya kuzindua kanuni za Baraza la Kiswahili la Taifa leo Jijini Arusha.


Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia) akimkabidhi zawadi mshindi wa bao Bwana Twaha Mohamed (kushoto) katika hafla ya uzinduzi wa kanuni za Baraza la Kiswahili la Taifa leo Jijini Arusha.


Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wajasiliamali wa kazi za sanaa za ufundi alipotembelea banda hilo leo Jijini Arusha.


Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akisikiliza maelekezo kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewange (kulia) alipotembelea banda la uchapishaji wa vitabu la Mkuki (Mkuki Publishers) leo Jijini Arusha.


Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Baraza la Kiswahili la Taifa mara baada ya kuzindua kanuni za Baraza hilo leo Jijini Arusha.

(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha)

……………………

Na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa ni muhimu kwa lugha ya Kiswahili kuwa na kanuni ambazo zitasaidia katika kufanikisha mawasiliano kwa jamii ili kuleta maendeleo chanya.

Hayo aliyasema leo Jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa kanuni za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) lengo ikiwa ni kuwazesha kusimamia matumizi ya lugha.

“Ni muhimu kwa kila lugha kuwa na kanuni na sifa kubwa ya lugha ya Kiswahili ni unyumbulifu, hivyo ninaamini kupitia kanuni hizi tutakuwa na usimamizi mzuri wa matumizi ya lugha hii” Dkt. Mwakyembe

Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa lazima kanuni hizo ziwe nyumbulifu na rafiki ili kuweza kuzifanyia marekebisho endapo kutakuwa na mapungufu yoyote wakati wa utekelezaji wake.

Pia aliwapongeza wataalamu wote kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali walioweza kufanikisha upatikanaji wa kanuni hizo na kuwataka kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kukuza, na kuendeleza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewange alilezea kuwa kuzinduliwa kwa kanuni hizo ni mojawapo ya mafanikio makubwa kwa lugha ya Kiswahili.

“Leo tunaweka historia nzuri katika nchi yetu kwa hatua hii muhimu ya kufanikisha uzinduzi wa kanuni za lugha ya Kiswahili ambazo pia zinatupa fursa ya kuwa na marekebisho kwa kadri zitakavyokuwa zinatekelezwa” Dkt. Sewange.



Historia inaeleza kuwa Baraza la Kiswahili la Taifa liliundwa na sheria ya bunge Na. 27 ya mwaka 1967 kwa shabaha ya kukuza, kuimarisha na kuendeleza Kiswahili nchini na baadaye kufanyiwa marekebisho mwaka 1983 kwa sheria ya Bunge Na. 7 ikiwa imepewa uwezo wa kufuatilia na kusaidia ukuzaji wa Kiswahili nje ya nchi na baadaye sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho ya mwisho mwaka 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...