Na Leandra Gabriel, Michuzi Tv

OFISA usalama wa shirika la Posta Tanzania  George Mwamgabe  anashikiliwa na  mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuhusika na usafirishaji wa dawa za kulevya kwa kutumia shirika hilo.

Mbali na ofisa huyo, mamlaka hiyo pia inawashikilia watuhumiwa wengine watano ambao nao wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Akizungumza leo Septemba 23, 2019 Kaimu Kamishina Jenerali wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya James Kaji amesema katika kipindi cha mwezi huu mamlaka hiyo imefanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya heroine katika Mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza pamoja na zaidi ya kilo 215 za vifurushi vya dawa za kulevya mirungi zilizokuwa zikisafirishwa kwa njia ya posta kutoka Arusha kwenda nchini Uingereza ameongeza.

Kuhusu kukamatwa kwa Ofisa wa usalama wa shirika la Posta, Kaimu Kamishina Jenerali James amesema, mtuhumiwa huyo awali alitoweka kufuatia mahojiano yaliyokuwa yakiendelea dhidi yake na Sasa yupo mikononi mwa mamlaka hiyo kwa kushirikiana na jeshi la polisi.

Akizungumzia kuhusiana na mirungi iliyokamatwa amesema uchunguzi wa kimaabara kutoka kwa mkemia mkuu wa serikali ulithibitisha majani hayo yana kemikali aina ya Cathinone ambayo inapatikana kwenye mmea wa mirungi.

Taarifa za awali zilibaini kuwepo kwa kasi kubwa ya usafirishwaji wa dawa za kulevya aina ya mirungi kutoka nchini kwenda nchi za Ulaya hasa Uingereza, Canada na Ufaransa kwa njia ya Posta ambapo awali vifurushi hivyo vilikuwa vikisafirishwa kupitia Posta ya Dar es Salaam na sasa vimekamatwa vikisafirishwa kupitia Posta jijini Arusha.

Mamlaka hiyo imetoa rai kwa wote wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya kuacha mara moja na kutafuta kazi halali za kufanya kwa kuwa mkono wa sheria utawafikia popote walipo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...