Na.Khadija seif, Michuzi tv

WAKALA wa usalama na afya Mahali pa kazi(OSHA)wameshauriwa kuongeza jitihada katika kusimamia viwango vya usalama na afya sehemu za kazi ili kuwezesha utekelezaji wa sera ya serikali ya uchumi wa viwanda kuwa na tija zaidi.

Akizungumza katika kikao kazi hicho,Katibu wa jukwaa la wahariri (TEF) ,Nevelle Meena amesema  wakala wa usalama na afya Mahali pa kazi (OSHA)  ina wajibu mkubwa katika kulinda Afya za wafanyakazi katika sekta ya umma,sekta binafsi pamoja na sekta isiyo rasmi, hivyo ni muhimu kwa taasisi hiyo kuhakikisha kwamba jamii ina uelewa wa kutosha kuhusu usalama wao wawapo kazini.

"Kikao hichi kimekua ni cha muhimu sana kwani wahariri au waandishi wa habari ni watu ambao wanakaa katika taasisi fulani iwe ya binafsi au ya umma au kati ya serikali na wananchi kwa ujumla hivyo wakala wa usalama na afya Mahali pa kazi (OSHA)    wameona kwamba wahariri wanaweza kuelimisha watanzania kuhusu kazi wanazozifanya, manufaa ya kazi wanazozifanya pamoja na faida ya wale wahusika kutekeleza matakwa, sheria ya usalama kazini,"

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa wakala wa usalama na afya Mahali pa kazi (OSHA) Khadija Mwenda ameeleza lengo la kikao hicho ilikua ni kubadilishana uzoefu na kuwafahamisha wahariri kuhusu namna ambavyo  (OSHA) inatekeleza majukumu yake ili kufanikisha suala zima la kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kuzingatia masuala ya usalama na afya sehemu za kazi.

"Changamoto kubwa inayotukabili kwa sasa ni uelewa mdogo kuhusu masuala ya usalama na afya miongoni mwa wadau na kwakutambua mchango mkubwa wa tasnia ya habari katika kuelimisha umma ndio sababu tumewashirikisha ili wao Kwanza wapate elimu ya namna gani sisi tunatekeleza majukumu yetu katika kusimamia nguvu kazi ya taifa na vile vile waweze kujua wanaporipoti masuala ya  (OSHA) basi wanaripoti katika mstakabali gani,"

Naibu Mtendaji Mkuu wa gazeti la jamhuri Manyerere Jackson amesema vikao vya namna hiyo vitasaidia sana kwa sababu wahariri sio malaika hawajui kila jambo na Kama wahabarishaji wakuu wa wananchi ni sharti la kwanza wao kuyafahamu mambo kiundani ili zile taarifa zinazofikiswa kwa jamii ziwe za uhakika.

"Wakala wa usalama na afya Mahali pa kazi (OSHA) ni taasisi kubwa yenye umuhimu wa kipekee katika uhai wa wafanyakazi nchini katika maslahi ya uchumi,"
      Kaimu Mtendaji mkuu wa OSHA Bi. Khadija Mwenda akiongea na wahariri mbalimbali toka Vyombo vya habari nchini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...