Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Lootha Sanare, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuchukua nafasi ya Dkt. Steven Kebwe ambaye uteuzi wake umeteguliwa.


Akitangaza uteuzi na utenguzi huo leo Septemba 20, 2019 Katibu mkuu kiongozi  Balozi Mhandisi John Kijazi, ameeleza kuwa Rais amefanya uteuzi na mabadiliko kadhaa.

Aidha Rais Magufuli amemteua Musa Masele ambaye alikuwa msaidizi wa mkuu wa mkoa wa Geita, kuwa mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Mkoani Morogoro.

Mbali na teuzi hizo pia Rais amefanya mabadiliko ambapo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Charles Kabeho, amehamishiwa wilaya ya Chato na Mkuu wa Wilaya ya Chato Msafiri Mtemi amehamishiwa Wilaya ya Tarime. 

Aidha, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi 12 watakaowakilisha Tanzania nchi mbalimbali, katika uteuzi huo wamo pia Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dk Modestus Kipilimba.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akisoma majina ya viongozi mbalimbali walioteuliwa ama waliobadilishwa vituo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 20, 2019 PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...