Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu 

TAASISI tatu nchini Tanzania zisizo za kiserikali wamemuomba Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC)Rais John Magufuli kuingilia kati kutafuta ufumbuzi wa sintofahamu inayoendelea nchini Afrika Kusini.

Wakizungumza leo Septemba 6,2019 , na waandishi wa vyombo vya habari viongozi wa taasisi hizo ambazo ni Action for Change(ACHA), The Right Way(TRW) na Mtandao wa Mashirika ya Kutetea Haki za Binadamu Kusini mwa Afrika(SAHRINGON) wamesema kuna kila sababu ya viongozi kuchukua hatua ya kukomesha machafuko yanayoendelea Afrika Kusini.

Akizungumza kwa niaba ya taasisi hizo, Martina Kabisama kutoka SAHRINGON amesema kwa pamoja wanatoa mwito kwa Mwenyekiti wa SADC Dk.Magufuli kuchukua hatua za haraka kukomesha ukatili unaofanywa nchini humo dhidi ya watu wa mataifa mengine ya Afrika.

"Wimbi la kushambuliwa kwa watu wanaoitwa wageni si peke linatokea Afrika Kusini, bali pia limetokea katika nchi mbalimbali katika ukanda wetu.Mfano siku za karibuni kuna mbunge mmoja nchini Kenya alitoa kauli inayoumiza kwa wale aliowaita wageni.

"Uzalendo ambao uliasisiwa na waasisi wa mataifa ya Afrika na mababa wa Afrika umevamiwa na kuufanya uzalendo usinyae."Ni suala la kupiga kengele kwamba Waafrika kwa pamoja waungane na kuanisha zaidi chanzo cha ubaguzi huu mpya unaobagua watu wa mataifa mengine , miongoni mwa watu wa mataifa,"amesema.

Kabisama ameongeza ACHA, TRW na SAHRINGON wanatambua kuwa Tanzania ndiye Mwenyekiti wa SADC , hivyo wanayo imani kuwa Rais wetu mpendwa Dk.Magufuli anaweza kuitumia nafasi aliyonayo kumaliza sintofahamu inayoendelea nchini Afrika Kusini.

"Tunatoa mwito wa mikakati ya kuvunja minyonyoro ya utengano wa namna hii ya unyanyasaji wa aina hii ambavyo vyote ni dalili ya kutengana na siyo kuungana-Muungano wa Afrika.

"Viongozi wa Afrika budi warejee uongozi uliotukuka(uongozi wa pamoja na wa mmoja mmoja) kujiamini na weledi, kutengeneza mitandao na viongozi wenzao wa Afrika...

"Ili kupambanua vikwazo kwa pamoja na kupambana kwa pamoja dhidi ya ubaguzi wa watu wa mataifa unaoota mizizi katika ukanda huu wa dunia,"amesema.

Kabisama amesema kile kilichotokea kwa kaka na dada zetu nchini Afrika Kusini ambapo raia wetu wa Afrika wa damu wanaumia kwa kiwango kikubwa kwa kunyanyapaliwa uto wao, haki zao za binadamu a fursa ya maendeleo yao ni fedheha kwa wanaotekeleza vitendo hivyo.

"Kinachotokea nchini Afrika Kusini na sehemu zingine za bara letu ni cha kihistoria ambapo machafuko ya ukatilii yameachwa bila kushughulikiwa na wahusika."Kwa mshangao wetu Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zilizoridhia na kusaini mikataba na mapatano ya kimataifa.

"Mathalani mkataba wa kimataifa wa kupinga aina zote za ubaguzi na mkataba wa kuondoa aina zote za unyanyasaji dhidi ya wanawake.Ziko wapi sheria za kimataifa huko Afrika Kusini?"

Ameongeza wakati wanatoa mwito huo kwa ajili ya kuvunja minyororo hiyo ya ubaguzi na kutengwa , pia wanatoa mwito kwa raia wa Afrika kusimama kidete kupigania amani endelevu na utulivu milele.

"Iwapo waafrika wanaota ndoto ya uzalendo wa Afrika , ndoto hiyo ni budi iwe kweli kupitia uhuru , usawa na mshikamano,"amesema Kabisama.
 Mratibu Taifa  wa Mashirika ya kutetea Haki za Binadamu kusini mwa Afrika (SAHRINGON),Martina Mnenegwa Kabisama akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar kuhusu kutoa mwito kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (SADC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli kuchukua hatua za haraka kukomesha ukatili unaofanywa nchini Afrika Kusini dhidi ya Watu wa Mataifa mengine.  Picha na Michuzi JR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...