Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe Alli Hapi akifungua kikao  cha kamati ya afya ya mkoa wa Iringa 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe Alli hapi wa tatu katikati waliokaa akiwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela wa pili kushoto katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikao cha afya cha mkoa

Na Francis Godwin, Iringa
MKUU wa mkoa wa Iringa Alli Hapi ameagiza ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Iringa kutoa taarifa sahihi kwa wananchi pale panapotokea taarifa za upotoshaji kuhusu chanjo zinazotolewa kwa Watoto ili kutovuruga zoezi la chanjo ya Surua ya surua Rubella itakayoanza kutolewa Septemba 26 hadi 30 mwaka huu .

Kuwa iwapo upotoshaji utapewa nafasi kwenye mambo ya msingi na wataalam wanaohusika na mambo ya kitaalam wakawa kimya ni hatari kwa wananchi kwani wanaweza kushindwa kupeleka Watoto kupatiwa chanjo hizo na mwisho wa siku madhara makubwa kwa Watoto yakajitokeza kwa kushindwa kupewa chanjo husika.

Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha siku moja cha kamati ya huduma ya afya ya msingi mkoa wa Iringa kilichofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu Huria mjini Iringa .

Amesema kuwa kuna uthibitisho wa kitaalam kwamba ni asilimia 85 tu ya Watoto wanaopata chanjo ya Surua wakati wanaotimiza miezi 9 kuwa wanapata kinga kikamilifu ya ugonjwa wa Surua .

Aidha kuna Watoto wengine ambao hawajapata kabisa huduma ya chanjo na kuna vituo vya huduma za afya ambazo hazijafikia lengo la kuwachanja Watoto kwa asilimia 100.

“ Mlundikano wa Watoto hawa wasio na kinga kamili kila baada ya miaka 3 hadi 4 huweza kusababisha milipuko ya ugonjwa wa surua ndio maana serikali imeamua kuifanya kampeni hii ili kuzuia mlipuko wa ugonjwa huo “ alisema Hapi

Kuwa kwa ajili ya kuwezesha zoezi hilo kuwa na mafanikio makubwa kama yaliyokusudiwa na serikali ya awamu ya tano ni vizuri lazimka elimu kwa jamii imeendelee kutolewa ili waone umuhimu wa kushiriki kampeni shirikishi ya surua Rubella .

Pia kuhamasisha ushiriki wa jamii kama viongozi wa ,wazazi na walezi kuhakikisha kila mlengwa anafikiwa katika eneo husika ,kusaidia kukanusha upotoshaji unaoweza kujitokeza kutokana na kampeni ya chanjo ya surua Rubella au chanjo kwa ujumla pamoja na kuhabarisha wananchi kuhusu madhara ya ugonjwa wa surua Rubella na polio kwa Watoto wenye umri wa wa chini ya miaka mitano kufika kupatiwa chanjo hiyo. 

Hivyo amewataka wakuu wa wilaya zote tatu za mkoa wa Iringa kusimamia zoezi la kampeni ya chanjo katika wilaya zao na kuhakikisha wanawafikia Watoto wote wanaostahili kupata chanjo hizo kwa asilimia 100.

Mkoa wa Iringa kama ilivyo kawaida yake ya kufanya vizuri na kuongoza katika kampeni mbali mbali za kitaifa umejipanga kufanya vizuri katika zoezi hili la chanjo kwa kuona walengwa wote wanafikiwa walipo .

“ Kampeni hii itafanyika kitaifa kwa siku tano kuanzia septemba 26 hadi 30 mwaka 2019 chanjo zitatolewa kwenye vituo vinavyotoa huduma za afya ya uzazi ,mama na mtoto na sehemu nyingine kama vile shule ,sokoni minadani na vituo vya mabasi kama ambavyo wananchi watakavyotangaziwa “

Hapi amesema anaipongeza wizara ya afya, maendeleo ya jamii jinsia ,wazee na Watoto chini ya ofisi ya tawala za mikoa na serikali za mitaa na wadau mbali mbali kwa kuchangia kufanikisha kampeni na huduma za chanjo kwa ujumla hapa nchini .

“Shukrani zangu kwa shirika la GAVI ,shirika la Afya ulimwenguni (WHO) ,shirika la kuhudumia Watoto (UNICEF, JHPIEGO CHAI ,JSI pamoja na wadau wengine kwa misaada yao ambayo imeweza kutufikisha hapa pia naishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutoa magari mawili ya kusambaza chanjo kwa Halmashauri ya Kilolo na Mafinga mji magari yaliyotolewa mwezi Septemba mwanzoni magari hayo yatasaidia sana kufakikisha kampeni hii “ alisema Hapi

Hata hivyo amesema kutokana na kazi kubwa inayofanywa na serikali ya Tanzania zimepelekea Taifa kuendelea kutokuwa na wagonjwa wa polio kwa zaidi ya miaka 23 sasa kwani mgonjwa wa mwisho kutolewa taarifa ilikuwa ni mwaka 1996 na mwaka 2015 Tanzani ilitangazwa kuwa miongoni mwa nchi zilizothibitika kutokuwa na ugonjwa wa polio.

Pia Tanzania imeshatangazwa kuwa ni nchi iliyothibitishwa kutokuwa na ugonjwa wa pepopunda kwa Watoto wachanga tangu mwaka 2011.

Mganga mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Robart Salim amesema kuwa mkoa unakusudia kuwachanja watoto 137,796 wenye umri wa miezi 9 hadi miezi 59 kwa chanjo ya surua Rubella na Watoto wenye umri wa miezi 18 hadi miezi 42 watapewa chanjo ya polio .

Pia amesema mkoa umejipanga kutoa mafunzo kwa wachanjaji 262 ,watunza takwimu 262 na wahamasishaji 131.

Nae Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela amesema kwa zoezi la chanjo ya mlango wa kizazi kwenye Halmashauri ya Iringa zilikwenda vizuri sana isipo kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ambao wamekuwa wakisuasua ila zoezi la chanjo ni jambo la msingi sana kwa Watoto hivyo kwa chanjo itakayoanza sasa atahakikisha Manispaa ya Iringa nayo inafanya vizuri .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...