Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo September 17 ametimiza ahadi ya ufadhili wa Masomo kuanzia Kidato cha Tano hadi Sita kwa Watoto wa kike 100 kutoka familia duni waliofaulu masomo ya Sayansi lakini wakashindwa kuendelea na masomo kwa kukosa Ada ambapo katika ufadhili huo amewalipia Ada na Vifaa ya shule ikiwemo Sare,mabegi, vitabu, madaftari na Nauli.

RC Makonda amesema lengo la ufadhili huo ni kumkomboa mtoto wa Kike kutoka familia duni aweze kupata elimu bora itakayosaidia kubadili maisha ya Familia na mwisho wa siku kuwa na Taifa lenye Wanawake Wanasayansi na Wagunduzi.

Aidha RC Makonda amesema ufadhili huo unaenda sambamba pia na kumuunga Mkono Rais Dkt.John Magufuli alieamua kumkomboa mtoto wa mnyonge kwa kutoa elimu bure kuanzia Darasa la Kwanza hadi kidato cha nne na yeye ameamua kupokea kijiti kwa kuwasomesha kidato cha tano na Sita ili wakifika vyuo vikuu wanufaike na Mkopo.

Hata hivyo RC Makonda amesema zoezi hilo litakuwa endelevu kila mwaka ambapo amewahimiza wanafunzi waliobahatika kupata fursa hiyo waitumie vizuri huku akimshukuru Balozi kwa Kumuunga mkono katika kampeni hiyo.

Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Bw. Khalfan Abdulrahman Al-Mazouqi amesema ufadhili huo ni Mwendelezo wa Kuunga Mkono juhudi za RC Makonda kwenye kila jambo kwakuwa amekuwa mtu wa kupigania maslahi ya Wananchi anaowaongoza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...