NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said-TABORA
MKUU
wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanry amewalinganisha walimu na silaha aina ya Katyusha
iliyotumiwa na majeshi ya Muungano wa Kisovyeti (Soviet Union) au Urusi
wakati wa vita Kuu ya Pili ya Dunia kwa vile huwa hawashindwi katika jambo
lolote.
Mhe.
Mwanry ameyasema hayo leo Septemba 16, 2019 Mkoani Tabora wakati akifungua
Kongamano la Walimu la “Amsha Amsha na
Mwalimu Bank” lililoandaliwa na
Mwalimu Commercial Bank kwa lengo la kutoa elimu ya fedha ikiwa ni pamoja na kujenga
hamasa kwa walimu kutumia huduma za benki hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa
inamilikiwa na walimu nchini.
“Katyusha
ni silaha iliyotumiwa na majeshi ya Muungano wa Kisovyeti (Soviet Union) au
Urusi kwenye vita Kuu ya Pili ya Dunia, na iliwapatia mafanikio makubwa katika
mapambano hayo, na mimi walimu wangu Mkoani Tabora huwa nawalinganisha na
silaha ya Katyusha kwani huwa hawashindwi kitu, wamenisaidia sana katika
kampeni mbalimbali za maendeleo hapa Tabora ikiwemo ile ya upandaji miti ambayo
imefanikiwa.” Alisema.
Alisema
kwa niaba ya serikali Mkoani Tabora na wananchi wa Mkoa wa Tabora na Walimu kwa
ujumla wako tayari wanaikaribisha benki ya Biashara ya Mwalimu mkoani humo
ikiwa ni pamoja na kutumia huduma zake.
“Wameona
isiwe tu kazi ya kufundisha darasani bali wameona wanasweza kutengeneza kitu
kinachoitwa Benki ya biashara ya Mwalimu, umoja ni nguvu na utengano ni
udhaifu, ukienda benki wao hawaangalii hivi mnavyofikiria wanaangalia umeingiza
kiasi gani na utachukua kiasi gani na umekopa shilingi ngapi na utarudisha
kiasi gani nawapongeza kwa kuwa na chombo hiki.” Alisema.
Kwa
upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard
Makungwa alisema, moja ya mikakati ya benki hiyo kwa sasa ni kuhakikisha
inawafikmia walimu nchi nzima na wameanza kwa kongamano kama hilo mkoani Kigoma
kwa nia ya kutoa elimu ya fedha lakini pia kujenga hamasa kwa walimu kutumia
huduma za benmi hiyo ambayo inamilikiwa na walimu kwa kiasi kikubwa.
“Benki
yetu sasa ina miaka mitatu tangu ianze shughuli zake, benki hii ni mali yenu,
tumieni huduma za benki yenu, tayari tuna matawi mawili Dar es Salaam, na
tumefungua ofisi kwenye mikoa ya Morogoro, Mwanza na Mbeya na tunakusudia
kufanya hivyo kadri muda unavyokwenda na ndio maana tuko hapa leo kuamsha amsha
mwalimu na benki yenu.” Alifafanua Bw. Makungwa ambaye alifuatana na Kaimu Mkuu
wa Biashara na Masoko, Bi. Leticia Ndongole na Mkurugenzi wa Fedha Bw. Selemani
Kijori.
Aidha
washiriki nao wamepongeza hatua ya uongozi wa benki kuwafikia huko mikoani na
kushauri kuwa benki lazima iwe karibu na wateja wake ili kujenga kuaminiana.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry, akifungua kongamano la walimu la "Amsha Amsha na Mwalimu Bank" Mkoani humo kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu Septemba 16, 2019. Kongamano hilo lililoandaliwa na Mwalimu Bank, lililenga kutoa elimu ya fedha kwa walimu ikiwa ni pamoja na kutoa hamasa kwa walimu kuitumia benki hiyo ambayo asilimia kubwa ya wanahisa wake ni walimu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Richard Makungwa.(kulia), akitoa hotuba yake kwenye kongamano hilo. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Tabora, Bw.Norbert Pandisha.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry, akifungua kongamano la walimu la "Amsha Amsha na Mwalimu Bank" Mkoani humo kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu Septemba 16, 2019. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Richard Makungwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Richard Makungwa.(kulia), akitoa hotuba yake kwenye kongamano hilo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Richard Makungwa.(kulia), akitoa hotuba yake kwenye kongamano hilo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Richard Makungwa.(kulia), akitoa hotuba yake kwenye kongamano hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry (kulia) na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mmoani Tabora (WCT), Bw. Norbert Pandisha, wakimsikiliza Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bw.Aron Masalu, (kushoto), wakati akitoa hotuba yake kwenye kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mmoani Tabora (WCT), Bw. Norbert Pandisha
Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bw.Aron Masalu
Baadhi ya walimu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanry (hayupo pichani).
Kaimu Mkuu wa Biashara na Masoko Mwalimu Commercial Bank Plc. Bi. Leticia Ndongole akitoa elimu ya fedha kwa washiriki.
Mshiriki akizungumza kwenye kongamano hilo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc. Bw. Richard Makungwa (kulia), akiwa na Kaimu Mkuu wa Biashara na Masoko wa benki hiyo. Bi. Leticia Ndongole wakisikiliza maoni ya washiriki. |
Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc. Bw. Richard Makungwa (katikati), akijadiliana jambo na Kaimu Mkuu wa Biashara na Masoko wa enki hiyo na Afisa Uhusiano, Bw. Said Rajabu wakati wa kongamano hilo.
Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo.
Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa.
Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Tabora, Bw.Norbert Pandisha, (wapili kulia), Katibu wa CWT Mkoa wa Tabora, Bw.Aron Masalu (watatu kulia), Mkurugenzi wa Fedha wa MCB, Bw.Selemani Kijori (kushoto) na Kaimu Mkuu wa Biashara na Masoko, Bi. Leticia Ndongole.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry (kulia), akifurahia jambo na Afisa Uhusiano wa benki hiyo, Bw. Michael Kachala
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...