Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha
KATIBU Mkuu wa ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamuhanga amezitaka halmashauri zote nchini ambazo bado zinasuasua katika kutekeleza sheria ya kutoa asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya vikundi vya walemavu, vijana na wanawake.

Amesema ili kuhakikisha wanatenga fedha zisiopungua asilimia 100 au zaidi kwa ajili ya kusaida vikundi na kubainisha kuwa serikali haita mfumbia macho mkurugenzi yeyote wa halmashauri ambaye atashidwa kutekeleza sheria hii ya kutenga fedha hizi kwa ajili ya kutoa mikopo kwa makundi haya.

Haya ameyasemwa katibu Mkuu wa ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamuhanga wakati alipotembelea kikundi cha watu wenyeulemavu cha Tumaini Ushiriki kilichopo wilayani Longido mkoani hapa ambapo alipata fursa ya kujionea mambo mbalimbali yanayofanywa na kikundi hicho ikiwemo unenepesha wa mbuzi kwa ajili ya kuwauza .

Amesema hii ndio njia pekee itakayosaidia serikali kuwawezesha wananchi wake kiuchumi na kuhahikisha wanainua kipato chao wanatengeneza ajira na wanakuza uchumi wa mwananchi na serikali kwa ujumla ili nchi yetu iweze kufikia viwango vya uchumi wa kati.

Hata hivyo ameungamkono kikundi Tumaini Ushiriki kikundi ambacho kinafanya kazi ya kunenepesha mbuzi kwa ajili ya kuwauza cha watu wenye ulemavu kwa kununua mbuzi moja ambaye aliwakabidhi kituo cha watoto yatima cha Namanga

Kwa upande wake katibu wa chama cha watu wenye ulemavu wilayani Longido ambaye pia ni mwanachama wa kikundi cha Tumaini Ushiriki, Emanuel Taraiya amesema ameiomba serikali kutenga bajeti kwa ajili ya kuwapa elimu watu wenye ulemavu.

Amesema wasikae ndani watoke nje wapaze sauti ili serikali iweze kutoa asilimia za fedha ambazo wametengewa kwa ajili ya mikopo ambayo itaweza kuwasaidia kwani walemavu wengi wamekuwa hawajui haki zao .

Kwa upande wake katibu wa kikikundi cha Tumaini Ushiriki Kitoitoi Ole Ndwati amesema kuwa kikundi chao kinafanya kazi ya kunenepa mifugo kwa ajili ya kuiuza katika masoko mbalimbali ,alisema kuwa kikundi chao kinaakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upande wa masoko kutokana na ushuru wa mifugo kupamba kwa kiasi kukubwa hali inayowafanya kukosa wateja wa kununua mifugo yao.

Amesema kuwa changamoto inayowakabili ni masoko pamoja na mazingira magumu ya kufanyia kazi, mitaji yao kuwa midogo, kauli au lugha chafu wanazotolewa na watu ambao sio walemavu hivyo ameiomba serikali kuwasaidia kutatua changamoto hizo ili nao waweze kufanya biashara na kunufaika.

Naye mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Longido mebainisha kuwa swala la kutoa mikopo kwa walemavu lazima atekeleze sheria ya kutenga fedha hizo kwa ajili ya kuwapatia kundi maalumu ambalo ni wanawake vijana na watu wenye ulimavu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...