Na Charles James, Michuzi TV

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Haki elimu, inayojishughulisha na kutoa elimu ya usawa kwa watoto wote katika elimu, limezindua utafiti uliofanyika na kituo hicho katika mikoa mitano(5) kujua changamoto zinazowakwamisha watoto wa kike katika kupata elimu katika Jamii zetu.

Akizindua utafiti huo jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia, Dkt Leonard Akwilapo, amesema serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na asasi za kiraia Kama Haki elimu, katika kuinua elimu hapa nchini na serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha watoto hasa wa kike wanabaki shule.

"Sisi Kama serikali tunatambua kazi kubwa mnayoifanya asasi za kiraia, hasa ninyi haki elimu, mnasaidia kueneza elimu kwa Jamii na kuhakikisha watoto wanabaki shule, na sisi serikali tunafanya kila jitihada kuhakikisha watoto hasa wa kike wanabaki shule" amesema, Dkt Akwilapo.

Serikali imekuja na mpango wa elimu bure kwa shule za awali hadi kidato cha nne yote haya ni kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu, sambamba na hilo tumejenga na tunaendelea kujenga mabweni ya watoto wa kike hasa katika shule za kata.

Amesema wameweka adhabu kubwa kwa mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kumbebesha ujauzito au kuoa mtoto lakini licha ya hiyo bado wataendelea kutoa elimu kwa Jamii juu ya umuhimu wa kumsomesha mtoto wa kike na faida zake

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Haki elimu, John Karage, amesema kupitia elimu wanayoitoa kumekuwa na mafanikio makubwa kwani mpaka sasa idadi ya udahili kwa watoto wa kike umeongezeka hadi kufikia asilimia 90, na Sasa kunakuwa na uwiano Kati ya watoto wa kiume na watoto wa kike katika udahili.

Amesema utafiti huo unalenga kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu na kuondokana na changamoto zinazowakumba, katika kupata elimu kwa mtoto wa kike.

Nae Dkt Mugisha Lucius, ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu Cha Dar es saalam, wakati akiwasilisha utafiti huo amesema utafiti huo umefanyika katika mikoa ya Dar es saalam, Kilimanjaro, Tabora, Dodoma na Lindi, huku akibainisha moja ya vikwazo kwa mtoto wa kike kwenda shule ni tamaduni za maeneo husika.

Akatolea mfano" Mkoa wa Lindi ni kwamba mtoto wa kike akifikisha umri flani anaondolewa nyumbani kwa wazazi na kupeleka nyumba ya karibu, ambapo kule anakosa malezi ya karibu ya wazazi hivyo kushindwa kupata elimu kikamilifu" amesema Dkt Mugisha.

Pia kukosekana kwa mahitaji maalumu kwa watoto wa kike imetajwa kukosesha watoto wa kike mda wa kusoma na hatimaye kuingia katika mahusiano Jambo ambalo hufifisha ndoto zao kabisa, pia mtoto anapo kuwa kwenye mzunguko wa siku zake watoto wengi hukosa masoma kutokana na kutokuwa na visitili vinavyotakiwa kwa mtoto wa kike.

Aidha Mkoa wa Tabora imetajwa kuwa kipindi cha kilimo cha tumbaku ndipo watoto wengi hushindwa kwenda darasani na badala yake wanajiingiza katika kilimo na kukosa mda wa masomo kwa watoto.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa ripoti ya utafiti kuhusu wasichana kushindwa kuendelea na masomo.
 Baadhi ya wanafunzi na wajumbe waliohudhuria hafla ya kuzindua ripoti ya utafiti kuhusu wasichana kushindwa kuendelea na masomo iliyofanyika jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, Dk John Kalaghe akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji, Dk Leonard Akwilapo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe baada ya kuzindua ripoti ya utafiti kuhusu wasichana kushindwa kuendelea na masomo. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...