Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB), Japhet Justine akielekeza jambo wakati wa mkutano na Wadau wa Pamba na Kahawa mkoani Simiyu katika kubadilishana uzoefu. 

Benki Ya Maendeleo Ya Kilimo (TADB) yakutana na Wadau wa Pamba na Kahawa mkoani Simiyu katika kubadilishana uzoefu. TADB, inayochagiza maendeleo ya kilimo nchini Tanzania imepata fursa ya kushiriki katika majadialiano juu ya fursa mbalimbali zilizopo katika mazao ya pamba na kahawa na mkakati uliopo katika kuendeleza mazao hayo. Majadaliano hayo yaliyofanyika mkoani Simiyu yakihusisha wadau mbalimbali ikiwemo serikali na pamoja na wadau wa maendeleo yaani shirika la Huduma za Kifedha (FSDT) na Gatsby Foundation wakiwa waandalizi wakuu katika majadiliano hayo.

Mkoa wa Simiyu, ni mojawapo ya mikoa yenye fursa nyingi za kuwekeza pamoja na ari yake ya kuleta maendeleo makubwa mkoani humo, Aidha Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ameeleza kuwa ‘’Simiyu ina rasilimali nyingi ikiwemo mifugo ya ng’ombe zaidi ya milioni 1.2 na wakazi zaidi ya milioni 1.7 ambao wengi wao wanajishughulisha na kilimo cha pamba, hivyo angependa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya maendeleo ya kilimo katika kusukuma ajenda hii ya maendeleo mkoani Simiyu na kuona kuwa wakulima wanafaidika kilimo hicho. Kwa maana mapinduzi ya uchumi wa viwanda yanaenda moja kwa moja na maendeleo kaika sekta ya kilimo, kwa kuwa malighafi nyingi zinatoka katika sekta hiyo’’
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya maendeleo ya Kilimo, Japhet Justine alieleza namna ambavyo benki ya maendeleo ya kilimo ina mkakati ambao umelenga kufanya mapinduzi makubwa ya zao la pamba na kuwawezesha wakulima wa chini wa pamba na kahawa pamoja na vyama vya ushirika (AMCOS) kuhakikisha kuwa wananufaika na kilimo cha pamba na na kuendelea kumiliki thamani ya zao mpaka linapofika kwa mlaji. 

Na sio tu kukusanya mazao kupitia vyama vya msingi na kuuza siku ya kwanza, bali kuanza kufungua mnyororo wa thamini na kushiriki kwenye fursa mbali mbali kabla ya kufikia ngazi kubwa ya masoko. Kwa mwaka 2017 pekee uzalishaji wa pamba ulikuwa tani 120,000, wakati kwa mwaka 2018 uzalishaji uliongezeka hadi Zaidi ya 220,000.  

Benki ya maendeleo ya kilimo kupitia Mkurugenzi Mtendaji wake ilishauriana na wataalam wa zao la pamba haswa pendekezo la kufanya mabadiliko ya pamoja ya kuongeza thamani katika hatua za awali katika chama cha msingi au chama kikuu kwa kuwezesha upatikanaji wa viwanda vya kutofautisha kati ya pamba nyuzi na pamba mbegu katika ngazi ya ushirika. Mabadiliko haya yataongeza tija kwa mkulima na pia kuongeza ajira na pia kubadilisha taswira ya ushirika. Akiongeza bwana Japhet Justine amependekeza Vyama Vya Msingi na Vyama Vikuu vibadilike na kujiendesha kifaida na isiwe kuajiri ya kukusanya mazao pekee. Tunaamini mpango huu ni endelevu kwa maendeleo ya wakulima wote, AMCOS na sekta nzima ya kilimo. 
Akiongelea zao la Kahawa, TADB imefanya mapinduzi makubwa mkoani Kagera. “Tuliweka Bilioni 23 Mwaka 2018 kuwezesha malipo ya awali kwa wakulima zaidi ya laki moja na elfu arobaini na mbili (242,000) na pia tumefanikiwa kufufua viwanda vidogo vya kukoboa kahawa na kuajiri zaidi ya wafanyakazi 5,200. Wakati huo huo tuliweka tena bilioni 7.1 kama sehemu ya kufufua vyama hivi vikuu vya ushirika. 

Mpaka sasa tunaweza kusema mwaka 2019, kama benki ya maendeleo ya kilimo ilivyoweza kuwekeza mkoani Kagera katika zao la kahawa kwa kutumia mfumo huu wa kuziwezesha AMCOS tatu tu na kuzipa sapoti ya uendeshaji na ushauri zaidi wa masoko ili waweze kufaidika na zao lao na kwa kushirikiana na mfumo jumuishi, leo hii wakulima wengi wanafaidika na zaidi ya watu 5000 wameajiriwa wakiwemo zaidi ya wanawake 1000. 

Benki ya maendeleo ya maendelo ya kilimo inawekeza kilimo kuanzia ngazi ya chini na kuwezesha mnyororo wa thamani ya mazao kupitia huduma za mbalimbali za kifedha. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...