Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Mchezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi habari kuhusiana na Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jumafest) litalifanyika Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAZIRI wa habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Herrison Mwakyembe ameutaka Umma wa watanzania kujitokeza kwa kushiriki kwenye tamasha la kimataifa la utamaduni wa Afrika mashariki (Jamafest) linalotegemea kufanyika katika Uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Septemba 21 hadi 28 mwaka huu.
Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo wakati wa mkutano wa Waandishi Habari kuhusiana tamasha hilo amesema matarijio ya nchi kuwa yetu kama mwenyeji wa tamasha ni pamoja kuvunja rekodi ya maonesho ya kuonyesha vipaji tulivyonavyo, kazi mbalimbali za mtanzania ikiwemo kuhifadhi na kulinda utamaduni wa mtu mweusi kupitia tasnia ya sanaa itakayo leta taswira ya kiushindani.
"Watanzania wote hapa nchini wahudhurie kwenye onesho kubwa la kitamaduni ambayo lengo letu ni kuonyesha roho ya Afrika ambyo ni utamaduni katika nyanja mbalimbali za sanaa," amsema Dkt.Mwakyembe
Dkt.Mwakyembe amesema kuwa tamasha hilo litawashirikisha wasanii na wajasiriamali kutoka nchi sita za Jumuiya ya Afrika mashariki zikiwemo Kenya , Uganda , Burundi, Rwanda na Tanzania kwa kuonyesha tamaduni za nchi zao.
Tamasho hilo limeratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Wizara ya habari Utamaduni Sanaa na michezo kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wa tasnia ya sanaa ili kuweza kufanikisha hilo.
Kwenye maadhimisho hayo wasanii wetu nchini wakiongozwa na Peter Msechu wameandaa wimbo maalumu utakaobaba ujumbe wa utamaduni wetu kwa ajili ya kulipamba tamasha hilo.
Dkt. Mwakyembe amesema tamasha hilo la kimataifa litawashirikisha wachonga vinyago, wabunifu wa mavazi,wasuka mikeka, watengenezaji wa nywele, wanamuziki wa dansi , watunga riwaya na michezo ya kuigiza.
Tamasha hilo litazinduliwa na Septemba 22 na Mmoja wa kiongozi wa juu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...