Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Addscoin Tanzania Limited, Japhet Raphael akizungumza na wamiliki, mameneja na wachimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

******************************
Wachimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wametakiwa kuchangamkia fursa ya mfumo mpya wa fedha wa bitcoin ili waweze kujinufaisha kiuchumi.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Addscoin Tanzania Limited, Japhet Raphael akizungumza na wamiliki na wachimbaji mji mdogo wa Mirerani, alisema hivi sasa dunia imebadilika hivyo jamii inapaswa kuchangamkia teknolojia hiyo.

Raphael alisema wachimbaji hao wanapaswa kuwekeza fedha kwenye mfumo huo ili kuendana na teknolojia hiyo mpya ya fedha ambayo inatumika dunia nzima.

“Mfumo wetu wa bitcoin wa kampuni ya Addscoin Tanzania unaweza kuwekeza kuanzia sh200,000 hadi sh50 bilioni na kujipatia faida kwa kila siku hivyo ni fursa nzuri,” alisema Raphael.

Alisema makao makuu ya kampuni hiyo yapo mtaa wa Msasani barabara ya Mwai Kibaki jijini Dar es salaam na jijini Arusha wapo jengo la Arusha Trade Centre barabara ya Sokoine.

Meneja wa Addscoin Tanzania, kanda ya kaskazini Amenye Mwakisambwe alisema yeye anafanya kazi kwenye mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga. 

“Tunawawezesha watu kumiliki Bitcoin kwa kununua package zake hivyo wachimbaji wa madini wanapaswa kuchangamkia fursa hii,” alisema Mwakisambwe. 

Hata hivyo, baadhi ya wamiliki na wachimbaji hao walidai kuwa bado elimu zaidi inatakiwa kutolewa juu ya kujiunga na mfumo huo.

Mmoja kati ya wachimbaji hao Samuel Lugemalila alisema uwazi unapaswa kuwepo juu ya suala hilo kwani baadhi ya makampuni yalifanya utapeli baada ya watu kuwekeza.

Mchimbaji mwingine Salum Ngoya alisema yeye ametambua kuwa taasisi hiyo inatumia mfumo wa bitcoin ambao upo sawa na mitandao ya fedha inayotumika kwenye simu za mikononi.

Mmoja kati ya mameneja wa migodi, Zephania Joseph alisema ameelewa utaratibu japo hajafahamu uwekezaji unavyoanza kuwekwa.

Mmiliki mwingine, Abubakary Madiwa alisema taasisi hiyo inapaswa kuwa na nyaraka za benki kuu ili watu waiamini zaidi na kuondokana na fikra potofu ya kutapeliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...