Wafanyabiashara 10 wa madini wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya ambako watano kati yao wamesomewa mashtaka tofauti ya uhujumu uchumi ikiwemo utoroshaji wa madini .

Katika kesi ya kwanza ambayo imesomwa mbele ya Hakimu Mkazi, Andrew Scoout inawahusu watumiwa watatu ambao ni Mike Konga, Sauli Solomon na Emmanuel Kessy ambao wamesomewa mashtaka matatu.

Akiwasomea mastaka yao Wakili wa Serikali, Basilius Namkambe amesema shitaka la kwanza ambalo linawahusu watuhumiwa wote watatu ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Alisema kuwa kati ya Juni Mosi na ‪Juni 30‬, mwaka huu watuhumiwa hao walijipatia fedha za Zambia kiasi cha Kwacha 290,000 kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa raia mmoja wa Zambia kwa kumuuzia dhahabu.

Wakili na Namkambe alisema kosa la pili la watuhumiowa hao ni utakatishaji wa fedha kiasi cha kwacha 290,000 ambazo walizipata kwa udanganyifu kutoka kwa raia wa Zambia.

Watuhumiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa Mahakam hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na Wakili Namkambe akadai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Andrew Scoult akaailisha kesi hiyo hadi ‪September 23‬ itakapotajwa tena mahakamini hapo.

Katika kesi ya pili, watuhumiwa wawilI, Mike Konga na Sauli Solomoni wamesomewa mastaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha mbele ya Hakimu Denis Luwongo.

Wakili wa Serikali, Basilius Namkambe ameiambia Mahakama kuwa watuhumiwa kwa pamija kati ya Juni Mosi na ‪Juni 30‬ mwaka huu walijipatia fedha kiasi cha dola za Marekani 115,000 kwa njia ya udanganyifu baada ya kumuuzia Henry Clever, raia wa Ujelumani amdini aina ya dhahabu kilo moja.

Wakili Namkambe alisema kosa la pili la watuhumiwa hao ni kutakatisha fedha kiasi cha dola za Marekani 115,000 ambazo walizipata kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa raia wa Ujerumani aitwaye Henry Clever.

Watuhumiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa vile Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Wakili wa Serikali, Basilius Namkambe alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakalika na akawasilisha maombi ya kutaka baada ya kuahilishwa kwa kesi hiyo, Mtuhumiwa wa Pili, Sauli Solomon achukuliwe na Jeshi la Polisi kwa ajili ya upelelezi.

Maombi hayo yalisababisha mvutano na wakili wa utetezi Baraka ambaye alisema kuwa mteja wake alikamatwa tangu Septemba Mosi mwaka huu na kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa mahojiano na muda wote huo alikuwa mikononi mwa Polisi, hivyo ni vema apelekwe gerezani na kama watamuhitaji kwa upelelezi wamfu

Hata hivyo Wakili wa Serikali, Namkambe alisema kuwa ombi lake ni sahihi kwa vile hata kama ni kumfuata huko ni lazima Mahakama itoe idhini hivyo ni busara aruhusiwe kwenda Polisi ili kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo kuepuka malalamiko yanayoweza kujitokeza baadaye kuhusu upelelezi kuchelewa kukamilika.

Hakimu Denis Luwongo akatoa uamuzi wa kuruhusu mshtakiwa kuchukuliwa na Polisi kwa ajili ya upelelezi na kuahilisha kesi hiyo hadi ‪September 23‬, mwaka huu.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...