Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanaokutana kuanzia leo Septemba 16, 2019 jijini Dar es Salaam. Picha zote na Matokeo Chanya+.
======= ========= =========
NCHI
za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), zipo katika mkakati
wa kuwa Mfumo Satelaiti ambapo utawezesha taarifa za nchi hizo
kudhibitiwa katika ukanda huo bila kuvuka mipaka.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe wakati wa ufunguzi wa
Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali
ya Hewa waliokutana jijini Dar es Salaam. Waziri Kamwelwe ameema kwa
muda mrefu nchi za SADC zimekuwa zikitumia mfumo wa Satelaiti ambao
unahitaji taarifa kwenda katika nchi za Ulaya na Marekani ndio zirudi
nchini na kumfikia muhusika hivyo wanataka kuondokana na utaratibu huo.
Amesema
maofisa hao waandamizi watatumia mkutano huo kujadili na kuja na
ubunifu ambao utarahisisha kila nchi mwanachama kusimamia mawasiliano
yake bila kutegemea uthibiti kutoka nje ambao sio salama kwa nchi na
watuamiaji.
“Mkutano
huu huu wa siku tano wa sekta ya Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya
Hewa ni mwanzo mzuri wa nchi za SADC kuweka mazimgira salama katika
mfumo wa ke wa taarifa na mawasiliano ya inteneti kwani tupo kwenye
mkakati wa ujenzi wa Satelaiti ya pamoja hivyo kuachana na mifumo ya
zamani,” alisema. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miundombinu SADC,
Mapolao Mokoena amesema mkutano huo utaweza kusaidia uelewa wa watendaji
wa Serikali kujua njia ya kupita katika kuifanya jumuiya ifikie malengo
yake hasa katika miundombinu. Mokoena alisema baadhi ya nchi zimeonesha
uthubutu katika ujenzi wa miundombinu akitolea mfano wa Tanzania hivyo
kuzitaka nchi zingine ziongeze jitihada katika eneo hilo ambalo ni
muhimu katika kukuza uchumi wan chi husika.
“SADC
ina program yake ya kuendelea miundombinu katika sekta zote hivyo
mkutano huu ni mwanzo mzuri wa utekelezaji huo ni imani yangu kuwa
tutaweza kufikia mazimio yenye tija kwa kila nchi mwanachama,” alisema.
Mkurugenzi huyo ambaye alimuwakilisha Katibu Mkuu wa SADC, Dk.Stergomena
Tax alisema sekta ya Tehama, Bahari, Uchukuzi na Hali ya Hewa ni sekta
muhimu katika kukuza uchumi hivyo ni vema kila nchi kuwekeza katika eneo
hilo.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi.
Mkurugenzi wa Miundombinu SADC, Mapolao Mokoena amesema mkutano huo utaweza kusaidia uelewa wa watendaji wa Serikali kujua njia ya kupita katika kuifanya jumuiya ifikie malengo yake hasa katika miundombinu.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi.
Viongozi wakifuatilia kwa makini.
Meza kuu.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe akicheza ngoma mara baada ya kumaliza kufungua mkutano.
Burudani ya Ngoma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...