Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa kufunga kongamano la Walimu wilayani Kasulu mkoani Kigoma
.Baadhi ya walimu wa Mkoa wa kigoma wakifiatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolijia Prof. Joyce Ndalichako wakati akifunga Kongamano la Walimu lililoandaliwa na Benki ya Biashara ya Walimu, Kasulu mkoani Kigoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na mmoja wa mwalimu aliyeshiriki Kongamano la Walimu lililoandaliwa na Benki ya Biashara ya Mwalimu, Kasulu Mkoani Kigoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akiteta jambo na Mkurugenzi wa Benki ya Biashara ya Mwalimu Richard Makungwa wakati wa hafla ya kufunga Kongamano la walimu lililoandaliwa na benki hiyo Kasulu, Mkoani Kigoma
Mkurugenzi wa Benki ya Biashara ya Mwalimu Richard Makungwa akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Kongamano la walimu lililoandaliwana Benki hiyo Kasulu, Mkoani Kigoma

…………….
Na Editha Karlo,michuzi tv,Kigoma


Waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia Prof,Joyce Ndalichako ameutaka uongozi wa Benki ya biashara ya Mwalimu MCB BANK kuboresha huduma za kifedha ikiwemo kuweka vivutio na masharti rafiki ambayo yatawawezesha walimu nchini kukopa fedha ili kukuza vipato vyao.

Prof,Ndalichako ametoa wito huo wakati akifunga Kongamano la walimu
wilayani Kasulu Mkoani Kigoma na kusisitiza kuwa matarajio ya serikali ni kuona benki ya biashara ya mwalimu inakuwa rafiki kwa walimu nchini kwa kuondoa adha na vikwazo ambavyo kwa muda mrefu walimu wamekuwa wakikabiliana Navyo katika taasisi mbalimbali za kifedha.

“Benki ya Biashara ya Mwalimu iwe na ahueni kwa mwalimu anapokuwa ni mteja katika kufanya hivyo walimu wengi watahamasika kujiunga na benki hii, kupitishia mishahara pamoja na hata kuchukua mikopo”

Aidha ameutaka uongozi wa Benki hiyo kusimamia vizuri fedha iliyokwisha wekezwa na walimu ili kuwavutia walimu wengine ambao bado hawajajiunga na kusisitiza kasi ya uanzishwaji wa ofisi za benki hiyo katika mikoa yote nchini iongezeke ili kuwavutia wateja.

” Nafahamu kwamba tayari mnatoa huduma kidijitali na mnashirikiana na Benki ya Posta kutoa huduma katika maeneo ambayo hamna ofisi na lakini ni muhimu mkaharakisha uanzishwaji wa ofisi zenu kila mkoa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma,,

Waziri Ndalichako pia amewaasa walimu nchini kuwa na Utamaduni wa kujiwekea akiba pindi wanapopata mishahara yao ili iwasaidie kuanzisha miradi mingine ya kiuchumi ambayo itakuwa mkombozi wa maisha yao pindi wanapostaafu.

“”Walimu tambueni akiba ni kile kitu unachokiweka kwanza kabla ya kuanza matumizi, lakini watu wengi wanadhani akiba ni bakaa baada ya matumizi kwa utaratibu huo kamwe hakutakuwa na kitu kinachobaki,,

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Mwalimu Richard Makungwa
amesema benki hiyo ime endelea kujiimarisha katika kusogeza huduma kwa wateja wake nakwamba tayari imeanzisha ofisi zake katika baadhi ya mikoa nchini ikiwemo MBEYA MOROGORO na MWANZA huku ishirikiana na Benki ya Posta kutoa huduma kwa wateja ambao bado mikoa yao haijafikiwa.

Amesema katika benki hiyo mwalimu mmoja mmoja anamiliki hisa takribani asilimia 35.28 huku chama cha walimu na kampuni yao wakimiliki takribani asilimia 16.17.

” ukiangalia utakubaliana nami kuwa chombo hiki ni cha walimu na madhumuni yake ni kuwaletea maendeleo wao wenyewe ndiyo maana tukasema lazima tuwafikia walimu popote walipo ,,alisema Mkurugenzi huyo.

Naye mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange amesema mara nyingi watumishi wanakosa nidhamu ya fedha na kutumia zaidi ya kile anachopata na kusisitiza kuwa ni vizuri walimu wakawa na utaratibu wa kujiwekea akiba ili pindi wanapostaafu waweze kuishi maisha ambayo wanaishi wakiwa kazini.

Nae mwalimu mstaafu aliyeshiriki kongamano hilo Kalist Tarimo ameishukuru Benki ya Biashara ya Mwalimu kwa kufanya Kongamano hilo ili kutoa elimu kwao lakini pia ameishaiuri benki hiyo kuwana na ofisi katika kila Wilaya ili walimu waweze kutumia huduma za benki hiyo.

Kongamano hilo limeandaliwa na Benki ya Biashara ya Mwalimu na limeshirikisha walimu kutoka Mkoa wa Kigoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...