Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akitoa hotuba yake katika sherehe za maadhimisho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Bodi ya Mapato (ZRB) sherehe hizo zilizofanyika leo huko Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Mapato (ZRB) Zanzibar Ndg,Saleh Sadiq Osman alipopkuwa akiwatambulisha wajumbe wa Bodi hiyo wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mapato (ZRB) zilizofanyika leo huko Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Mapato (ZRB) Zanzibar Ndg,Saleh Sadiq Osman katika sherehe za maadhimisho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Bodi ya Mapato (ZRB) sherehe hizo zilizofanyika leo huko Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar Baadhi ya wafanyakazi wa Idara mbali mbali za Bodi ya Mapato wakiwa katika sherehe maalum za maadhimisho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Bodi ya Mapato (ZRB) zilizofanyika leo huko Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mapato na waalikwa mbali mbali wakiwa katika sherehe maalum za maadhimisho ya kutimia miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Bodi ya Mapato (ZRB) zilizofanyika leo huko Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akimkabidhi cheti Mwanafunzi Khairia Mnyanja Simai Skuli ya Benmbele akita mshindi wa Insha Mdahalo wa kuhusu umuhimu wa kulipa Kodi katika sherehe za maadhimisho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Bodi ya Mapato (ZRB) sherehe hizo zilizofanyika leo huko Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Feda na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akimkabidhi cheti Mwanafunzi Ishaka Ali Dadi Skuli ya Fidel Castro Pemba akita mshindi wa Insha Mdahalo wa kuhusu umuhimu wa kulipa Kodi katika sherehe za maadhimisho ya kutimia miaka 20 ya kuanzishwa kwa Bodi ya Mapato (ZRB) sherehe hizo zilizofanyika leo huko Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Feda na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa.[Picha na Ikulu


………………..

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amesema ukusanyaji mzuri wa mapato unaofanywa na taasisi za kukusanya kodi umeiwezesha serikali kupunguza utegemezi wa bajeti katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo.

Dk. Shein amesema hayo katika hafla ya kuadhimisha miaka 20 ya Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), iliofanyika Makao makuu ya taasisi hiyo Mazizini Jijini hapa.

Alisema mapato yaliokusanya na taasisi za ZRB na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) katika mwaka 2018/2019 ya shilingi Bilioni 727, yameifanya serikali kupunguza utegemezi wa bajeti kutoka asilimia 30.3 mwaka 2010/2011 hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka 2019.

Alisema kiwango hicho kinadhihirisha jinsi Serikali ilivyopindukia malengo yaliowekwa katika Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020, Ibara 68-d, iliyobainisha uwezo wa taasisi hizo wa kukusanya jumla ya shilingi Bilioni 800 ifikapo mwaka 2020/2021.

“Uwezo wetu umeimarika ambapo mwaka 2018/2019 ZRB pekee ilikusanya wastani wa shilingi Bilioni 36.6 kwa mwezi”, alisema.Dk Shein alisema wakati alipoingia madarakani mwaka 2010, mapato yaliokusanywa na ZRB na TRA yalikuwa wastani wa shilingi Bilioni 13.5 kwa mwezi, huku ZRB pekee ikikusanya shilingi Bilioni 8.7 pekee.

Alisema serikali imefanikiwa kutekeleza mikakati mbali mbali ya kuimarisha utendaji na uwezo wa taasisi hiyo katika kukusanya mapato, ambapo katika mwaka 2014/2015 ilikusanya wastani wa shilingi Bilioni 16.17

Rais Dk. Shein alibainisha kuwa kutokana na ukusanyaji huo mzuri wa mapato, Serikali imeweza kuimarisha maslahi ya wafanyakazi mara nne, kutoa pensheni jamii kwa kila mzee aliefikia umri wa miaka 70 nchini pamoja na kuimarisha huduma mbali mbali za kijamii, ikiwemo afya na elimu.

“Tunapoweza kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege na bandari, tunaponunua vifaa vya utibabu na badhi ya huduma nyengine kubwa ikiwemo utoaji wa ruzuku katika pembejeo na zana za kilimo ni uthibitisho wa kuongezeka pato letu nchini”, alisema.

Alisema kurahisisha kazi ya ukusanyaji wa mapato, kuna umuhimu wa kuwaelimisha wananchi kuzifahamu vyema sheria za kodi zilizopo ili waweze kuzifuata kwa uamilifu.

Alisema ni wajibu wa Bodi ya mapato kuhakikisha inapanga utaratibu maalum wa kuwaelimisha wananchi juu ya sheria za kodi ili waelewe wajibu wao, viwango vinavyopaswa kulipwa, wapi wakalipe na wakati upi.

Aidha, alisema Wizara ya Fedha na Mipango na Bodi zinazoshughulikia ukusanyaji wa kodi zinapaswa kuwa na wataalamu waliobobea ili waweze kufanyakazi katika taasisi za Uwekezaji.

Alisema baadhi ya wamiliki wa hoteli hawalipi kodi ipasavyo kwa mujibu wa viwango vinavyopaswa kulipwa na kubainisha kuwa hiyo ni changamoto inayopaswa kushughulikiwa pamoja na wafanyabaishara wanaokodisha nyumba za wageni.

“Tuelekeze juhudi zetu katika matumizi ya teknolojia na mbinu za kisasa katika ukusanyaji na ulipaji kodi”, alisema.Katika hatua nyengine, Dk. Shein aliwataka wafanyakazi wa taasisi za kukusanya mapato kuendelea kufanyakzi kwa uadilifu na uzalendo na kusisitiza umuhimu wa matumizi ya lugha nzuri, sambamba na kutoa huduma kwa kuzingatia wakati wawapo kazini.

Aidha, aliitaka ZRB kuandaa mazingira mazuri pamoja na miundombinu ya kisasa kwa lengo la kurahisisha ukusanyaji na ulipaji wa kodi pamoja na kuhakikisha wafanyakazi wana taaluma za kutosha.Alibainisha kuwa njia bora zaidi katika kupata ufanisi kazini ni kuhakikisha kuna wakusanyaji kodi waliosomea fani mbali mbali zinazohusu ukusanyaji na ulipaji wa kodi.

Mapema, Waziri wa Fedha na Mipango. Balozi Muhamed Ramia aliwakumbusha wafanyakazi wa ZRB dhima waliyonayo ya kufanyakazi kwa uangalifu na kuepuka changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika mazingira yao ya kazi.Alisema kazi ya ukusanyaji wa kodi inahitaji hekima na busara, kwa kutambuwa kuwa wateja wao ni watu wenye tabia tofauti.

Nae, Kamishna Mkuu wa ZRB, Joseph Abdalla Meza, alisema kwa nyakati tofauti uongozi wa ZRB umekuwa ukiwakumbusha wafanyakazi umuhimu wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia uadilifu na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Alisema malengo ya taasisi hiyo hivi sasa ni kujengo jipya la ghorofa nne katika eneo la Gombani kisiwani Pemba ili kuimarisha utendaji.Aidha, alisema miongoni mwa mikakati na mipango ya taasisi hiyo iliyotekelezwa na kufanikisha makusanyo mazuri ya mapato ni pamoja na kufanya tafiti saba mbali mbali.

Alisema katika kipindi chote tangu taasisi hiyo iundwe, imefanikiwa kujenga mashirikiano na taasii mbali mbali ikiwemo TRA, mashirika pamoja na Benki, hususun katika suala la kubadilisha uzoefu.

Meza, alisema changamoto kubwa inayoikabili taasisi hiyo ni ile ya baadhi ya wamiliki wa Hoteli kutoainisha viwango halisi vya tozo wanazotoza wageni pamoja na kushindwa kutoa risiti wakati wa mauzo, au kutoa risiti zisizo na uhalisia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...