Walimu pamoja na Wanafunzi wa Skuli ya Glorious Academy wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa kitengo cha Uchambuzi wa Athari zitokanazo na Chakula wa Wakala wa Chakula na Dawa (ZFPA)Aisha Suleiman wakati akitoa Elimu ya Matumizi ya Chakula Vinywaji pamoja na Peremende kwa Wanafunzi wa Skuli ya Glorious Academy Mpendae mjini Zanzibar.
Mkuu wa kitengo cha Uchambuzi wa Athari zitokanazo na Chakula wa Wakala wa Chakula na Dawa (ZFPA)Aisha Suleiman akitoa Elimu ya Matumizi ya Chakula Vinywaji pamoja na Peremende kwa Wanafunzi wa Skuli ya Glorious Academy Mpendae mjini Zanzibar.
Mkuu wa kitengo cha Ukaguzi wa Wakala wa Chakula na Dawa Mohamed Shadhil Shauri akitolea ufafanuzi baadhi ya maswala wakati akitoa Elimu ya Matumizi ya Chakula Vinywaji pamoja na Peremende kwa Wanafunzi wa Skuli ya Glorious Academy Mpendae mjini Zanzibar. 

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.


Na Miza Kona Maelezo Zanzibar 23/10/2019

Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar imepiga marufuku kutumia bidhaa ambazo vifungashio vyake havina maandishi ya lugha iliyokubalika kutumika kisheria nchini.

Akitoa elimu kwa wanafunzi wa skuli ya Glorious Acedemy huko Mpendae kuhusiana na uvumi uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu pipi na chokleti zimeingia nchini kuwa zina madhara Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa Athari zitokanazo na Chakula Aisha Suleiman amesema ni marufuku kutumia bidhaa kama pipi na chokleti ambazo maandishi yake yameandikwa kwa lugha isiyofahamika.

Amesema hakuna pipi ama chokleti zinazoingizwa nchini ambazo zina madhara wala athari kwa jamii bali ni kuzingatia vifungashio, viambata vilivyomo katika bidhaa na muda wa kumalizika kwake.Ameeleza Wakala wa Chakula na Dawa ina jukumu la kuhakikisha kwamba vyakula vinavyoingia nchini viko salama kwa matumizi ya binadamu na havileti madhara kwa mtumiaji.

Mkuu huyo amewafahamisha wanafunzi hao kuwa waangalifu wanaponunua bidhaa zenye vifungashio kwa kuangalia vyema maelezo yaliyomo ili kuepuka kupata madhara. Aidha Mkuu huyo amewataka wanafunzi hao kuacha kutumia vyakula vyenye sukari kwa wingi ili kuepukana na maradhi mbali mbali na kupata taifa lililoimara.

Aidha amesisitiza wanafunzi hao kutosikiliza taarifa za uvumi uliopo na kuwa walimu kwa wenzao ili jamii iondokane na jambo hilo. Nao wanafunzi hao wamesema kuwa wataitumia vyema elimu waliyoipata na kuwa walimu wazuri kwa wenzao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...