Anaandika Abdullatif Yunus, Michuzi TV KAGERA.

Miongoni mwa majengo saba ya Vituo vya Umahiri (Centers of Excellence) yanayojengwa hapa Nchini, chini ya Wizara ya Madini likiwemo jengo lililojengwa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, limekabidhiwa rasmi na kupokelewa na Waziri mwenye Dhamana Mhe. Dotto Biteko mapema Oktoba 04, 2019.

Jengo hilo lenye Orofa tatu, lenye thamani ya Sh. Bilioni 1.081 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyetaka kuona mabadiliko katika Sekta ya madini kwa kuweka mazingira wezeshi.

Akizungumza kabla ya kukabidhiwa jengo hilo, Waziri wa Madini  Dotto Biteko amepongeza usimamizi wa Jengo hilo kwa ujumla, huku akikumbusha nia ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutaka kujengwa kwa Vituo hivyo Saba, lengo likiwa kuifanya Sekta ya madini iwe sekta ya wadau na wachimbaji wa uhakika, na kuondokana na ujanja ujanja uliokuwa ukifanywa awali, kufuatia nia hiyo pamoja na mambo mengine tayari leseni 12000 zimefutwa na zitagawiwa Kwa wachimbaji wadogo, huku miongoni mwa hizo leseni, leseni 156 ni kutoka Mkoani Kagera.

Aidha Waziri Biteko ameongeza kuwa mpaka sasa Masoko zaidi ya 28 yameanzishwa na vituo vidogo zaidi ya 18 vya kununua madini vimefunguliwa,  ambapo utaratibu mwingine wa kupata cheti cha uasilia kwa ajili ya kuanza kupeleka madini hayo nje yakiwemo ya TIN  umekamilika na kufikia mwishoni mwa Mwaka huu Wizara itaanza kusafirisha madini nje ya Nchi, Hivyo kukamilika kwa jengo hilo ni fursa kwa wachimbaji na wafanyabiashara kuongeza ufanisi katika shughuli zao, na kuwataka kulitumia jengo hilo kwa malengo yaliyokusudiwa.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema nia ya Mkoa ni kuongoza Mikoa yote katika ukusanyaji madini, kwa kutoa elimu kwa wachimbaji wa madini wadogo na wakubwa bila kutumia nguvu kubwa, ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi huku suala la kudhibiti utoroshaji wa madini likizidi kuimarishwa, na wito ukizidi kutolewa kwa wawekezaji wa biashara ya Madini kuendelea kwekeza katika Sekta hii ya Madini Mkoani Kagera.

Jengo hilo lenye Ofisi za Maafisa madini na wataalamu, Ukumbi wa mikutano, eneo la mafunzo, Chumba maalumu la kuhifadhi madini (strong room) pamoja na huduma nyinginezo tayari limekabidhiwa kwa Wizara ya Madini kutoka kwa Wajenzi wa Jengo hilo Shirika la Suma JKT, na tayari Wizara imekabidhi kwa Tume ya Madini Mkoa wa Kagera tayari kwa matumizi.
 Pichani Waziri wa Madini Dotto Biteko akikabidhi funguo kwa Tume ya Madini mara baada ya kukabidhiwa toka Suma JKT ambao ndio wajenzi 
 Pichani In meneja mradi kutoka shirika la Suma JKT Kapteni Fabian Buberwa akiwasilisha taarifa yake mbele ya Viongozi kabla ya kukabidhi mradi wa jengo la umahiri.
 Pichani Waziri wa Madini Dotto Biteko akipokea funguo toka kwa Meneja mradi Kapteni Fabian Buberwa kama ishara ya kukabidhiwa Jengo la umahiri mara baada ya Kumalika ujenzi wake.
 Pichani Ni Msafara wa Waziri wa Madini Dotto Biteko ukiwasili kukabidhiwa jengo la Umahiri, baada ya kukamilika kwa ujenzi.
Pichani ni Mhe. Ditto Biteko Waziri wa Madini akitoa nasaha zake mapema kabla ya kukabidhiwa Jengo la umahiri.
 Pichani Bi Veronica Nangale Kaimu Meneja Mradi akiwasilisha taarifa ya Ujenzi kwa Viongozi mapema kabla ya kukabidhiwa kwa Jengo la umahiri.
Pichani ni Muonekano wa Jengo la Orofa Tatu lenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.081 lilojengwa Mkoani Kagera, chini ya Wizara ya Madini likiwa tayari kwa matumizi baada ya kukabidhiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...