Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Bi. Comfort King-Giboie akisisitiza jambo mbele ya timu ya Afya ngazi ya Mkoa (RHMTs) juu ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata miongozo (IPC guideline) katika Mkoa wa Kigoma.
Wataalamu wa Afya ngazi ya Mkoa wakifuatilia kwa makini mafunzo ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata miongozo ya IPC, yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika lisilo Lakiserikali la MSH kupitia mradi wa MTaPS.
Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Erick Kinyenje akitoa mafunzo ya namna yakuchanganya dawa za kuua vijidudu mbalimbali katika maeneo yakutolea huduma za Afya.Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chaote aakieleza jambo mbele ya Watoa huduma za Afya ngazi ya Mkoa, wakati wa mafunzo ya namna bora yakujikinga dhidi ya maambukizi mkoani Kigoma.


Na WAMJW – KIGOMA

Watumishi wa Sekta ya Afya nchini, wameaswa kufuata miongozo na taratibu za utoaji huduma za Afya wakati wa kutoa huduma kwa mgonjwa (IPC Standards) ili kupunguza tatizo la usugu wa wadudu dhidi ya dawa.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chaote, wakati akifungua mafunzo ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata miongozo (IPC Guidline) wakati wa kumuudumia mgonjwa Mkoani Kigoma.

Dkt. Paul Chaote amesema kuwa usugu wa dawa ni moja kati ya tishio kubwa kwa Afya ya binadamu nchini, huku akidai kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) limeshauri nchi wanachama kuanzisha mikakati ya kukabili dhidi ya tatizo hili.

“Usugu wa dawa umekuwa moja ya tishio kubwa kwa Afya ya Wananchi katika jamii, hivyo Shirika la Afya Duniani (WHO) linashauri kuanzishwa kwa afua/mikakati mbali mbali ili kuweza kupambana na tatizo hili la usugu” Alisema Dkt. Paul Chaote.

Dkt. Paul Chaote aliendelea kusema, matumizi ya dawa yasiyo na ulazima yanaweza kupelekea tatizo la usugu wa wadudu dhidi ya dawa, huku akisisitiza kufuata miongozo ya njia za kukinga (IPC Standards) wakati wa kumuhudumia mgonjwa, kama njia kuu ya kupambana dhidi ya usugu wa wadudu dhidi ya dawa.

“Kufuata miongozo ya IPC (Infection, Prevention, Control) ni njia yenye gharama nafuu ambayo tunaweza kuifanya, ambayo itakuwa msaada mkubwa katika lengo letu la kupambana dhidi ya usugu wa wadudu dhidi ya dawa” Alisema Dkt. Chaote.

Naye, Afisa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Boniface Marwa amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa watu 700,00/ hufariki Dunia kutokana na tatizo linalosababishwa na usugu wa wadudu dhidi ya dawa, huku akidai kuwa asilimia 89% ya vifo hivyo hutokea Barani Afrika na Asia.

Aliendelea kwa kusisitiza kuwa jitihada za makusudi ni lazima zichukuliwe na kila mtaalamu katika Sekta ya Afya ili kupambana na tatizo hili linalozidi kuwa tishio Duniani, huku akisisitiza juu ya kufanya tafiti mbali mbali ili kupata dawa mpya zitazoweza kupambana na wadudu sugu.

“Takribani watu 700,000 hufariki Duniani, kutokana na tatizo la usugu wa wadudu dhidi ya dawa, na asilimia 89% ya vifo hivyo hutokea Barani Afrika na Asia” Alisema Dkt. Boniface Marwa.

Kwa upande wake Afisa kutoka Kitengo cha Uhakiki Ubora, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Erick Kinyenje amewataka Wataalamu kutoka Sekta ya Afya mkoa wa Kigoma kuhakikisha wanapeleka Elimu juu ya muongozo wa kudhibiti na kukinga magonjwa (IPC Guidline) walioipata kwa watumishi wenzao katika maeneo yao ya kutolea huduma za Afya ili kukinga maambukizi katika maeneo hayo.

“Niwaombe mtusaidie kuifikisha Elimu hii mlioipata hapa kwa wWataalamu katika maeneo yenu yakutolea huduma za Afya, na kuisambaza miongozo hii ya njia bora za kukinga na kudhibiti maambukizi ya magonjwa katika maeneo hayo, hii itasaidia kupunguza maambukizi na jambo litalosaidia kupunguza usugu wa wadudu dhidi ya dawa”, alisema Bw. Erick Kinyenje.

Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Management Science for Health (MSH) kupitia mradi wa Medicines, Technology and Pharmaceutical Services (MTaPS), yanatarajia kuendelea katika mikoa yote iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola ili kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...