Kutokana na kuongezeka kwa tatizo la kiharusi nchini Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanzisha kitengo maalumu ili kuwachunguza na kuwapatia tiba stahiki wagonjwa wanaopata tatizo la kiharusi nchini. 

Hayo yamesemwa na Daktari Bingwa na Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu, Ubongo na Uti wa Mgongo hospitalini hapa, Dkt. Mohamed Mnacho wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya kiharusi duniani inayoadhimishwa Oktoba 29 kila mwaka. 

“Kwa siku Hospitali ya Taifa ya Muhimbili inapokea wagonjwa wa kiharusi kati ya 3 hadi saba ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wagonjwa hawa Muhimbili imeanzisha kitengo maalumu cha kuwahudumia wagonjwa wa kiharusi,”amesema Dkt. Mnacho. 

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), ugonjwa wa kiharusi ni wa pili na kwamba unasababisha vifo kwa asilimia 11.8 baada ya magonjwa ya moyo. 

Dkt. Mnacho amefafanua kwamba kiharusi ni ugonjwa wa tatu unaosababisha ulemavu kwa watu mbalimbali kwa asilimia 4.5 duniani na hivyo kusababisha watu washindwe kufanya shughuli za kila siku kutokana na kuongezeka kwa magonjwa ya kiharusi. 

Akizungumzia tatizo la kiharusi, Dkt. Mnacho amesema kuwa Kiharusi kinawapata zaidi watu wenye umri zaidi ya miaka 65, ingawa kwa sasa inaonekana pia tatizo hili linawapata watu wengi wenye miaka 45 au chini ya miaka 45, hivyo tatizo hili hivi sasa siyo la watu wenye umri mkubwa pekee yake. 

Dkt. Patience Njenje ambaye naye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu, Ubongo na Uti wa Mgongo wa Muhimbili, amesema zaidi ya asilimia 90 ugonjwa wa kiharusi husababishwa na shinikizo la damu. Lakini pia, magonjwa ya moyo, selimundu pia huchangia mtu kupata kiharusi. 

Kutokana na kuongezeka kwa ugonjwa wa kiharusi, Dkt. Njenje amewashauri wananchi kwenda hospitalini haraka kwa ajili ya kuipatiwa matibabu na amewashauri watoa huduma wa vituo vya afya ambako hakuna vifaa tiba vya kutosha kuwapeleka wagonjwa kwenye hospitali za rufaa ili wapatiwe haraka matibabu ya ubingwa wa juu. 

“Kiharusi husababishwa na mishipa ya damu kwenye ubongo kuziba au kupasuka, hutokea kwa haraka na matibabu yake ni ya haraka, hivyo mtu anapopata kiharusi ana saa 4 hadi sita kwa madaktari kuamua kupona au kusababisha ulemavu hivyo watu wanapaswa kuwahi haraka hospitali,” amesema Dkt. Njenje. 

Aidha Dkt njenje ametoa wito kwa watanzania kuweka utaratibu wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kugundua magonjwa yanayoweza kusababisha kiharusi na kuyadhibiti mapema kwa kunywa dawa na kubadilisha mfumo wa maisha. 



Naye Dkt. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu, Ubongo na Uti wa Mgongo kwa watoto, Dkt. Zameer Fakih amesema kuwa takwimu za dunia zinaonyesha kuwa mtoto mmoja kati ya watoto 4,000 wanaozaliwa kila siku hupata kiharusi na sababu kubwa ya kupata kiharusi kwa watoto ni magonjwa ya moyo na selimundu. 
Daktari Bingwa na Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu, Ubongo na Uti wa Mgongo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Patience Njenje akizungumza na waandishi habari kuhusu siku ya kiharusi ambayo huadhimishwa duniani Oktoba 29 kila mwaka. Kulia ni Daktari Bingwa na Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu, Ubongo na Uti wa Mgongo kwa watoto, Dkt. Zameer Fakih na Kushoto ni Daktari Bingwa na Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu, Ubongo na Uti wa Mgongo, Dkt. Mohammed Mnacho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...