Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
KATIKA kuendelea kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere viongozi na taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi wameendelea kuenzi kwa vitendo tunu alizotuachia baba wa taifa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililofanyika katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam Kamanda wa wa chuo cha mafunzo ya ulinzi wa anga Brigedia Jenerali  Mbaraka Mkeremy amesema kuwa Mwalimu aliamini jeshi dogo lenye uwezo wa kulinda nchi na kusema kuwa usalama, ulinzi na amani haviwezi kutenganishwa na dhana nzima ya maendeleo.

Amesema kuwa jeshi lililoanzishwa na Mwalimu Nyerere  mwaka 1964 lilikuwa dogo na liliundwa kwa kuzingatia misingi ya ujamaa na kujitegemea na lugha ya Kiswahili na Muungano vikawa ndio vitu vilivyoliweka jeshi hilo katika nafasi nzuri hadi leo.

Mkeremy amesema kuwa; Jeshi limeendelea kuishi kwa kumuenzi kwa vitendo  Mwalimu Nyerere licha ya dhana ya usalama kuwa pana na kukutana na chagamoto mbalimbali.

Akieleza changamoto zinazoikumba dhana nzima ya usalama ni pamoja na kutokuwepo kwa Mwalimu ambaye alisimamia misimamo yake pamoja na kizazi cha sasa ambacho ni sawa na asilimia 75 ambao hawajui historia ya Mwalimu.

"Asilimia 75 ya watanzania ni vijana waliozaliwa  miaka ya 1980 hiki ni kizazi kipya ambacho hawajaishi maisha ya Mwalimu, hawajui historia yake na wameathiriwa na utandawazi ambao unawafanya waishi kwenye taifa lao wakiwa na viongozi na wasipoangaliwa tutashindwa kuwandaa kuja kuwa viongozi wa baadaye "ameeleza.

Aidha ameeleza kuwa changamoto nyingine ya kiusalama ni hisia za udini, kukosekana a kwa ajira hasa kwa vijana wasomi, mitandao ya kijamii, hali tete za kiusalama katika nchi jirani hali inayopelekea kuongezeka kwa wakimbizi nchini, hisia katika suala la muungano  pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimaendeleo inayotekelezwa nchini kutofurahisha mataifa mengine.

Amesema kuwa Jeshi la Tanzania lipo makini zaidi katika kuhakikisha amani nchini inaendelea kudumu kama Baba wa taifa alivyosimamia misingi amani, ulinzi  na usalama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...