Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

FAMILIA ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura imeshindwa kuzuia furaha yao na kujikuta ikipiga makofi mahakamani baada ya Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu kumuachia huru kiongozi huyo wa zamani wa TFF.

Pamoja na kuachiwa huru mahakama imemtaka Wambura kulipa fidia ya Sh 100,998,121 kwa awamu tano.

Hatua hiyo, imekuja baada ya upande wa mashitaka kumfutia Wambura mashitaka ya uhujumu uchumi na kumsomea mashitaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo alikiri kutenda kosa hilo.

Akisoma adhabu hiyo, hakimu mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Kelvin Mhina amesema mshitakiwa atatakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu tano kuanzia leo, Sh. Miliini 20, Desemba 31, mwaka huu ( Sh 20,249,531), Machi 31,2020, Juni 30 na Septemba 30, 2020 ambapo fedha atakazotakiwa kulipa ni Sh 20,249,531 kama ilivyopangwa kwa miezi.

Aidha mahakama imemtaka mshitakiwa kutokufanya kosa lolote la jinai kwa miezi 12 na kwamba rufaa ipo wazi kwa asiyeridhika.

Kabla ya kutolewa adhabu, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai hawana rekodi ya makosa ya nyuma ya mshitakiwa hivyo, aliomba mahakama itoe adhabu kulingana na makubaliano ili iwe fundisho kwake na wengine.

Kwa upande wake , Wambura amedai hilo ni kosa lake la kwanza hivyo, ameiomba mahakama impe adhabu itakayomsaidia kushiriki kufanya shughuli nyingine za kijamii.

Mapema, akisoma makubaliano hayo, Wankyo amedai kuwa wameingia makubaliano na mshitakiwa huyo baada ya kukiri kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu hivyo wameamua kuondoa mashitaka ya kughushi, kutoa nyaraka za uongo na utakatishaji fedha ambayo ni mashitaka ya uhujumu uchumi na kwamba Wambura na upande wa serikali wamekubaliana kulipa fedha yote kwa awamu tano.

Baada ya kusoma makubaliano hayo, Hakimu Mhina alimuapisha mshitakiwa na kumuuliza kama alisaini kwa hiari yake na kudai alifanya hivyo kwa hiari yake.

Akisoma mashitaka mapya, Wakili Simon alidai Julai 6,2004 na Oktoba 30,2015 maeneo ya Ilala kwa udanganyifu Wambura alijipatia Sh 100,998,121 kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa lengo la kuonesha malipo ya mkopo wa Dola za Marekani 30,000 kutoka Kampuni ya Jekc System Limited.

Katika maelezo ya awali, Simon alidai Wambura kipindi hicho akiwa katibu Mtendaji wa TFF, Novemba 28,2002 waliingia makubaliano ya mkopo wa Dola za Marekani 30,000 lengo kufadhili michuano ya Chalenji kipindi hicho mwenyeji alikuwa Tanzania.Alidai Wambura alisaini makubaliano hayo kwa niaba ya TFF na kwamba walitakiwa kurudisha fedha zote pamoja na riba ya asilimia tano mara baada ya mashindano kukamilika.

Alidai Januari 13,2014 Kampuni ya Jekc System Limited iliandika barua kwa mshitakiwa na kwa njia ya udanganyifu Wambura aliilaghai TFF kwa kujaribu kuonesha alichaguliwa na kupewa mamlaka ya kisheria kukusanya fedha hizo kwa niaba ya TFF.

Wambura alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo akiwa na mashitaka 17 ikiwemo ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kutoka nyaraka za uongo na utakatishaji fedha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...