Na Leandra Gabriel, Michuzi TV 

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa akimaliza muda wa kuitumikia nafasi aliyochaguliwa na Rais Dkt. John Joseph Magufuli hatapata tabu kurudi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuendelea kufundisha masomo ya sheria kama awali. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililoandaliwa na Uongozi Institute kwa kushirikiana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Kabudi amesema kuwa katika awamu hii ya tano cheo ni dhamana na yeye hatapata tabu kurudi chuoni hapo wakati ukifika . 

"Mwenda tezi na omo....Marejeo ngamani, sitapata tabu kurudi chuoni hapa kwa kuwa katika awamu hii cheo ni dhamana na sitakuwa wa kwanza wala wa mwisho. Chuo cha Dar es Salaam ni nyumbani, nikimaliza ngwe hii nitarudi kwa mbwembwe" ameeleza Prof. Kabudi. 

amesema kuwa wakati tukimuenzi baba wa taifa lazima tukumbuke tunu alizotuachia ambazo zilikuwa katika mfumo wa kiitikadi na uadilifu, amesema kuwa masuala ya utu, usawa, uwajibikaji, uadilifu, uzalendo, maadili na umoja ndio mambo yanayoendelea kuliweka taifa letu kuwa kisiwa cha amani na utulivu na ni vitu ambavyo Mwalimu Nyerere ametuachia. 

vilevile amesema kuwa miaka 20 bila Mwalimu Nyerere taifa limeendelea kumuenzi hasa katika uongozi wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli na Serikali kwa ujumla wameendelea kuthamini na kusimamia misingi aliyoiweka Mwalimu ili kuhakikisha taifa linabaki salama na kuwa maendeleo endelevu. 

"Miaka 20 baada ya Mwalimu kifo cha Mwalimu tunu zimeendelea kuimarishwa kupitia Serikali ya Rais Magufuli, masuala kama maji, elimu, afya na uimarishwaji wa miundombinu mbalimbali umeendelea kuimarishwa katika maeneo mbalimbali nchini" ameeleza. 

Prof. Kabudi amesema kuwa viongozi lazima wafuate miiko na maadili katika kuwatumika wananchi bila kujali vyeo vyao bali kwa kuzingatia maadili, uwajibikaji ili kuweza kumuenzi Mwalimu kwa vitendo zaidi. 

kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na vyama vya Siasa akiwemo katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Bashiru Ally, Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Anna Makinda, Jaji Damiani Lubuva na viongozi wa dini na taasisi mbalimbali. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...