Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amesema kilo 1,444 za korosho zimekamatwa kutoka kwa wanunuzi wa kangomba katika operesheni maalum ambayo imeanza jana.

Akizungumza na baadhi ya wananchi eneo la maheha alisema kuwa serikali Ina nia njema na wakulima wa korosho kwakuwa utaratibu wa kangomba unawapunja .

"Kangomba marufuku ndani ya Wilaya yetu,kikosi Cha operesheni ya kukamata wanunuzi wa kangomba tayari limeanza kazi rasmi  na kilo 1444 zimekamatwa," alisema Waryuba

Amesema wananchi wanatakiwa kupeleka korosho zao kwenye vyama vyao vya msingi, na kwama maghala yapo wazi kupokea mzigo 

"Zoezi hilo ni endelevu na ndiyo limeanza,ambapo maeneo walioanzia  ni Kijiji Cha  maheha na Likorombe ndipo zilipopatikana kilo hizo,wananchi tusikubali,"alisema Waryuba.
Baadhi ya wananchi wa eneo la maheha,Wilaya ya Tandahimba wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba ,Mhe. Sebastian Waryuba alipokuwa akizungumza nao kuhusu suala la Kangomba na mambo mengine kuhusiana na Wakulima wa Korosho wilayani humo.

 Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba akishuhudia upimwaji wa Korosho za Kangomba zikipimwa kwenye Ghala la chama cha msingi Maja katika kijiji cha Maheha,wilayani humo
 Korosho za kangomba zikipimwa kwenye ghala la chama Cha msingi Maja  Kijiji Cha Maheha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...