NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

WAZIRI Mkuu Mstaafu ,Mizengo Pinda ameusisitiza mkoa wa Pwani ,kupitia viwanda vilivyopo mkoani humo kujikita kutumia raslimali na malighafi zinazotokana na kilimo kama silaha ya kuwaondoa wakulima kwenye lindi la umaskini .

Aidha ameitaka jamii kusomesha vijana wao ili kupata wasomi waliobobea katika fani mbalimbali kwa lengo la kupata watu sahihi wa kuendeleza viwanda vinavyojengwa kwa kasi nchini pasipo kuwaachia vijana kutoka nje ya nchi.

Akifunga maonyesho ya pili ya bidhaa za viwanda na wiki ya viwanda, yaliyofanyika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani, Pinda alisema ,katika kukuza uchumi wa viwanda,  awamu ya tano inaendelea kutekeleza mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano .

Alieleza ,kwa kuzingatia hilo, serikali imesimamia ukuaji wa uchumi wa kujenga uchumi na msingi wa viwanda hasa zinazotumia malighafi zinazopatikana nchini.

Pinda alielezea ,moja ya adui ni umaskini katika maeneo ya vijijini kwa asilimia zaidi ya 70 ambako ndipo kuna wafugaji,wakulima na wavuvi ambao kila kukicha wanapigana na umaskini.

"Kutokana na hilo vijikite katika kutumia raslimali inayotokana na wakulima kwani itasaidia na ni silaha ya kuwaondoa kwenye umasikini"alifafanua Pinda.

Alisema ,mkoa huo upo juu na unaitendea haki sekta ya viwanda na uwekezaji hivyo kuwepo kwa viwanda vinavyofunganisha maendeleo ya watu italeta tija kwa maslahi yao.

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alisema ,maonyesho ya mwaka huu yamefanikiwa tofauti na mwaka jana kwani viwanda 329 vikubwa,vidogo na vya kati vimeshiriki na watu wamejitokeza kutembelea na kununua bidhaa mbalinbali.

Ndikilo alieleza, hadi sasa mkoa huo una jumla ya viwanda vikubwa,vya kati na vidogo 1,192 na kutoa ajira ya moja kwa moja zaidi ya 20,000.

"Chimbuko la kuanzisha maonyesho haya yalitokana na kilio cha wawekezaji kukosa masoko na kusababisha hasara ,kuhatarisha ajira na kufungwa kwa baadhi ya viwanda  na vingine kutofahamika uzalishaji wanaoufanya"alifafanua Ndikilo.

Mkuu huyo wa mkoa alimuomba Pinda, kuwa balozi wa kuusemea mkoa ndani na nje ya nchi kutokana na kasi ya kuwa ukanda wa viwanda ili kuinua uchumi na pato kitaifa.

Awali mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani, Ramadhani Maneno aliiasa jamii kujenga utamaduni wa kupenda na kununua bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda vilivyopo Pwani.

Maneno pia alieleza ,Pwani ni sehemu ya kuwekeza na hakuna urasimu ,na kwa upande wa chama hii ni sehemu ya mkakati wake wa mwaka 2015-2020 ,huku vipaombele vyake ni kuona utekelezaji wa ilani kuhusiana na kuinua sekta ya viwanda na uwekezaji unafanikiwa.

Pamoja na hilo ,mwakilishi kutoka CRDB Rosemary Kazimoto alibainisha ,maonyesho hayo yamedhaminiwa na taasisi ya kifedha ya CRDB kwa kiasi cha sh.milioni 60.
 WAZIRI Mkuu Mstaafu ,Mizengo Pinda akizungumza jambo kwenye moja ya banda la Idara ya Uhamiaji alipokuwa akiyatembelea  wakati wa kufunga  maonyesho ya pili ya bidhaa za viwanda na wiki ya viwanda, yaliyofanyika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...