TANGU Rais Dkt John Pombe Magufuli, alipotembelea ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti hivi karibuni na kuangiza ujenzi huo uwe umekamilika ndani ya miezi mitatu ijayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameendelea kusimamia ujenzi huo usiku na mchana.

Usimamizi huo unaonekana kuanzaa kuzaa matunda ya haraka jambo ambalo sasa anadai kufurahishwa na kasi ya ujenzi huo kiasi cha kumpa matumaini ya kukamilika ndani ya miezi mitatu iliyotolewa.

Akizungumzia ujenzi huo, Makonda amesema kuwa, katika jambo ambalo Watanzania walifanya kwa isahihi na kwamba hawatakuja kujuta kufuatia maendeleo yake, ni pamoja na kumchagua Rais Magufuli kuwa rais wa nchi hii.

Kwa maana hiyo uamuzi wa kufanya hivyo hakika wanatakiwa kutambua kuwa walichagua maendeleo ya ujenzi wa miundombuni sahihi kama, mabarabara,Hospitali,shule na sasa machinjio makubwa na ya kisasa kabisa ya vingunguti.

Kwa maana hiyo anawaomba watanzania waendelee kuunga mkono juhudi zake kwani yeye na viongozi wengine hawatachoka kumsaidia ili kufikia malengo bora aliyokusuhudia kuwafanyia watanzania wote kipindi chote cha uongozi wake. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...