Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii  
Katika kumuenzi baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere, Shule ya Sekondari ya Makongo imefanya  shughuli mbalimbali  katika Hospital ya Mwananyamala ikiwa ni pamoja na kufanya usafi Kuchangia Damu na kutoa kutoa msaada wa Maji .

Shughuli hiyo  imeanza kwa maandamano na imeongozwa na mbunge wa Kinondoni Abdallah Mtulia kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Daniel Chongolo.

 Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumaliza kutembelea Hospitali hiyo na kukabidhi misaada mbali mbali Mkuu wa Shule ya Makongo, Kanali Yuda Kitinya amesema kuwa lengo kubwa la kufanya zoezi hilo ni kuwafundisha wanafunzi wa shule hiyo uzalendo  kama baba wa Taifa alivyokuwa akifundisha ambae alikuwa  anasisitiza uzalendo  katika nchi.

"Tunawafundisha vijana wetu uzalendo ili wafahamu kwamba ukiwa kijana unajukumu la kujitoa kwa ajili ya jamii inayokuzunguka kwani ninaimani kama tukiwafundisha na wakaelewa basi wataendelea kuelimisha wenzao na kujitoa siku hadi siku katika maisha yao yote".amesema Kanali Kitinya.

 Amesema, wanafanya yote hayo kwa ajili ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa tangu alipofarikiwa miaka 20 iliyopita.

Kwa upande wake, Mbunge wa  Kinondoni, Mtulia  ameupongeza uongozi mzima wa Shule ya Makongo kwa kufanya kitendo cha uzalendo kama hicho ambacho kinagusa jamii nzima, na pia kuwafundisha vijana uzalendo na moyo wa kusaidiana na kuwa na uzalendo.

"Kitendo hiki ni cha kuigwa na watanzania wote katika kumuenzi Baba wa Taifa kwa kufanya mambo yale mazuri aliyotuagiza na aliyotuachia ukizingatia amefanya mambo mengi sana ambayo hayatasahaulika kamwe" amesema Mtulia.

Amesema Baba wa Taifa kabla hajafariki alikuwa akihimiza sana upendo na kusaidiana na pia alileta sera ya ujamaa na kujitegemea. "Tunamuenzi Mwalimu Nyerere katika  kazi zake hasa katika mambo ya viwanda  na  afya kwani Mwalimu alijenga viwanda vingi sana vidogo na vya kati bila ya kusahau Kiwanda cha silaha cha nyumbu" amesema.

Aidha ameongeza kuwa katika kumuenzi baba wa Taifa tukumbuke pia siasa zake safi na uongozi bora. Pia amewaasa 

Naye Kaimu mganga mfawidhi wa hospital ya  Mwananyamala, Dkt. Isidory Kiwale amesema msaada huo utawasadia  kwa kiasi kikubwa hususani damu kwa kwani  upungufu wa damu imekuwa changamoto kubwa katika   sekta ya afya.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makongo (JWTZ), Kanali Yuda Kitinya na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (katikati) wakikabidhi Maji kwa ajili ya Watoto Njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala iliyopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni Kumbukizi ya Miaka 20 tangu kutokea Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, anayepokea kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt.  Isdory Kiwale.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makongo (JWTZ), Kanali Yuda Kitinya (wa pili kutoka kulia) na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (wa kwanza kutoka kulia) wakifanya usafi wa mazingira katika baadhi ya maeneo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam mapema leo.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makongo (JWTZ), Kanali Yuda Kitinya (kushoto) akielezea Nembo ya Shule hiyo ilichorwa katika Hospitali ya Mwananyamala baada ya Shule hiyo kutoa misaada mbalimbali katika moja ya Wodi ikiwa ni sehemu ya Kumbukizi ya miaka 20 tangu Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Kulia ni Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia
 Maandamano ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Makongo kutoka Bamaga jijini Dar es Salaam hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala katika kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tangu kutokea Kifo chake miaka 20 iliyopita.
Maandamano ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Makongo (JWTZ) na baadhi ya Askari Jeshi hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...