Charles James, Michuzi TV

KUELEKEA uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu, Spika wa Bunge, Mhe Job Ndugai amewataka watanzania kuwaamini wanawake na kuwachagua ili waweze kuwatumikia.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dodoma alipokua akitoa taarifa ya semina iliyoandaliwa na Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola.

Amesema semina hiyo itafanyika kuanzia Oktoba 26 hadi 29 mwaka huu jijini Arusha ambapo lengo lake ni kuhamasisha wajumbe wake kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu wanawake hususani katika eneo la uchaguzi.

Semina hiyo itashirikisha washiriki takribani 50 kutoka katika Nchi 18 za Jumuiya ya Madola ambapo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

" Kauli mbiu ya semina hii ni Kuboresha ushiriki wa Wanawake katika michakato ya uchaguzi. Ambapo pamoja na mambo mengine ni kuboresha ushiriki wa Wanawake katika michakato ya uchaguzi na hatimaye kuongeza idadi ya wanawake katika vyombo vya maamuzi hususani Bunge.

Tunafahamu zipo changamoto nyingi ambazo zinakwamisha wanawake kushiriki katika michakato ya uchaguzi kama wapiga kura na wagombea, changamoto hizo zote zitajadiliwa katika semina hiyo," Amesema Spika Ndugai.

Amesema wanatarajia kuwa na wageni mbalimbali katika siku hiyo ya ufunguzi wakiwemo Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Mabalozi wa Nchi 17 za Afrika ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola, Balozi wa Uingereza nchini, Balozi wa Pakistan nchini, Mawaziri na viongozi mbalimbali wanawake, Viongozi wa Dini, baadhi ya watendaji wa Serikali za Mikoa na Wilaya na wawakilishi kutoka UN Women nchini.

" Wanawake wana uwezo mkubwa sana wa kiuongozi, wengi waliopata nafasi walionesha uwezo walionao. Ni matarajio yetu tutafikia asilimia 50 kwa 50 ndani ya Bunge kama tutaendelea kuwaamini, siyo bungeni tu hadi kwenye vyombo vingine vya kimaamuzi.

Uchaguzi unaokuja wa Serikali za Mitaa ukatumike pia kuchagua viongozi walio bora hasa kwa kuzingatia nafasi ya Mwanamke kwenye uongozi, tuwaamini wanaweza," Amesema Spika Ndugai.
 Spika wa Bunge, Mhe Job Ndugai akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu semina ya wajumbe wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Nchi wanachama za Jumuiya ya Madola utakaofanyika jijini Arusha kuanzia 26-29 Oktoba mwaka huu.
 Spika wa Bunge, Mhe Job Ndugai akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake leo wakati akitoa taarifa ya semina ya Wabunge  kutoka Mabunge ambayo ni Wanachama wa Jumuiya ya Madola.
Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumzia semina ya Wabunge Wanawake kutoka Mabunge wanachama wa Nchi za Jumuiya ya Madola itakayofanyika jijini Arusha Oktoba 26-29 mwaka huu. Kulia ni Naibu Spika, Dk Tulia Ackson mwingine ni Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...